Serikali ya Kenya imezindua kampeini ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa upooza Septemba 23, 2011.Kampeni hiyo inalenga maeneo ambaye dalili ya ugonjwa huu imeanza onekana,kama vile Migori, Homa-Bay, Kisii, Nyamira na Transmara. .watoto walio chini ya miaka mitano watachanjwa.
Hivi majuzi waziri wa Afya ya Umma, Beth Mugo alitangaza kuwa Kenya inakabiliwa na hatari ya mkurupuko wa ugonjwa wa kupooza baada ya kijana mwenye umri wa miaka mitatu kupatikana virusi ya polio katika Wilaya ya Rongo, Mkoani Nyanza.
Ugonjwa wa polio husababiswa na virusi na kwa hivyo ni vingumu kutibiwa, punde tu mtu anapoambukizwa.
Mwongozo wa shirika la Afya duniani(WHO) unabainisha kuwa ili kudhibiti mzunguko wa virusi pori vya ugonjwa wa kupooza,ni muhimu kutoa chanjo za zaidi kwa njia ya kampeni kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 angalau kwa awamu mbili.
Chanjo hii inatolewa na wataalam wa afya kwa njia ya matone kinywani kwa watoto wote, bila kujali kama walipata chanjo hiyo hapo awali au hawakupata.
Adhari za ugonjwa wa kupooza(polio)
Akiwa na umri wa miaka ishirini na tano John Katana anaugua ugonjwa wa kupooza.Katana ni mmoja kati ya wakenya wengi ambayo,endapo wazazi wao wangeliwapeleka kuchanjwa, hii leo wangekuwa na uwezo wa kutembea bila matatizo yeyote.
Yeye hutumia kiti cha kukokotwa kwani miguu yake miwili imepooza.
Alipozaliwa mamake hakutilia maanani umuhimu wa chanjo hii.Hivyo basi,hakumpeleka kupata viwango vyote vinne vya chanjo ya kupooza.
Aliwaza kuwa,mwanawe na pia watoto wa jirani yake wamerogwa. Kijiji pale pia maradhi haya yalienea kwa kasi.huku Watoto zaidi ya kumi wakiabukizwa.
Dalili za polio
Mamake katana anasema mwanawe alianza kuumwa na kichwa, maumivu na udhaifu wa misuli.
Kwa bahati nzuri,kampeni dhini ya ugonjwa wa kupooza ilitangazwa na serikali. Baadya ya mafuzo ya kiafya,Akagundua kumbe mwanawe alikuwa tu anaugua polio kwa sababu ya uzembe kwake.
Laiti angalijua, Katana hangelemaa;angekuwa na afya nzuri kama watoto waliopokea chanjo wakiwawachanga.
Kwa sasa, yeye na akina mama wenzake wamechukua jukumu la kuwaelimisha wanawake umuhimu wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza.
Jinsi polio inavyoenezwa
*Watoto ambao hawajachanjwa
*virusi vya polio huenezwa kwa kula chakula au kunywa maji machafu yalichanganyika na virusi vya polio au kwa kinyesi cha mwadhiriwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni