Jumatano, 28 Septemba 2011

Ovarian Cancer(saratani ya mfuko wa mayai)


Hii leo nitaandika zaidi na kuwaelimisha kuhusu saratani ya mfuko wa mayai yaani ovarian cancer.

Je wajua kuhusu Saratani ya kifuko cha mayai ya uzazi ?
Mwanamke ana vifuko viwili vidogo vilivyo kila upande wa  mfuko wake wa uzazi.Kwa mujibu wa tafiti,ni vigumu kuitambua saratani hii.

Hivyo basi ni muhimu kutembelea daktari kila mwaka kwa uchukuzi wa kina.Dalili zake huonekana ugonjwa ukiwa umeenea mno.

Walio  kwenye hatari ya kupata saratani hii ni

v     -Wanawake wenye zaidi ya umri wa miaka 50 wako hatarini ya kuambikizwa ugonjwa huu.

v     mwanamke tasa
v     Ikiwa umewahi kuwa na saratani ya matiti
v     Ikiwa kuna mtu wa familia ambaye amewahi kuugua ugonjwa huu.
v     Kupata hedhi katika umri mdogo

Hata hivyo, kama saratani yingine,inapogunduliwa mapema mtu anaweza kupona.

Ni muhimu kula vyakula kama mboga, matunda ambavyo vinafahamika kupunguza hatari ya saratani.

Ni vigumu kupata takwimu kamili za akina mama wanaougua ugonjwa huu au maafa kwani Wanawake wengi hasa wa mashinani, wanafariki bila kufahamu wanaugua saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi.

Pia gharama ya kujitibisha ni ya juu mno.Hivyo basi ni wachache wana uwezo wakugharamia matibabu ya Saratani.

Zaidi ya hayo, kuna haja ya kuelimisha akina mama umuhimu wa kutafuta matibatu au kuchunguzwa katika sehemu ya uzazi mara kwa mara.

Wizara ya Afya pia ina jukumu ya kufanya kampeini ili kuukabili au kuangamiza ugonjwa wa saratani nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni