Kuna haja ya kutoa elimu ya afya ya uzazi shuleni.Ili kupunguza ongezeko la Ujauzito
Kwa vijana wakiwa wadogo.
Kulingana na mila na tamaduni za kiafrika baadhi wa walimu na pia wazazi hawataki kuzungumzia maswala ya ngono kwa watoto.
Hizi ni mila ambazo zimepitwa na wakati na ni jukumu letu kulitilia maanani elimu ya afya ya uzazi.
Kulingana na watalamu ya afya, unaweza kutungwa mwanamke au msichana mimba anapokaribia kupata hedhi kufanya tendo la ndoa pasipo kutumia mbinu yoyote ya kuuzuia.
Hivi majuzi visa vya wasichana wa chini ya miaka kumi kutunga mimba vimeripotiwa nchini Kenya.
La kusikitisha ni kwamba wengi hawana habari kuhusu afya ya uzazi
Pia waohupata matatizo ya kujifungua kwani viungo vyao kama vile mishipa ya uzazi haijakomaa.
Zaidi ya hayo,ugonjwa wa fistula unaweza ukatokea baada ya kujifungua.
Kwa hivyo elimu ya afya ya uzazi ni muhimu zaidi kwa kundi hili la vijana wasichana kwa wavulana.
Hivyo basi, kuna haja ya walimu shuleni, pamoja na wataalamu wa afya kutoka serikalini na mashirika binafsi kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana na wavulana ili waweze kuepuka matatizo yayoweza kuwakumba wakiwa wadogo.
Kulingana na elimu ya kisayanisi, wavulana wanapobalehe wanaweza kutoa mbegu za uzazi zenye uwezo wa kutunga ujauzito.
Hii ni wazi kuwa wavulana, hata wakiwa kwenye miaka kumi na kuendelea, wanaweza kumtunga msichana au mwanamke ujauzito!
Jinsi ya kujiepusha kupata mimba?
Kuijikinga kwa kutumia mbinu au mikakati tofauti ya upangaji uzazi
Kutojihuzisha na tendo la ngono kabla ya kuingia katika ndoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni