Mazingira machafu ni chimbuko la magonjwa chungu nzima.
Mamia ya watu kote duniani, huadhirika kiafya na hata kufariki kufuatia hali hii.
Hivyo basi, ni jukumu la kila mtu kuhakikisha ya kwamba hali ya usafi unadumishwa kila wakati.
Kwa mfano ugonjwa wa kipindupindu unahatarisha maisha ya watu wengi.Waswahili husema kuwa kuzuia ni bora kuliko kuponya.Fauka ya hayo, itakuwa ni jukumu ya kila mtu kuhakikisha anaishi katika mazingira safi,ilikuepuka magonjwa kama hayo.
Kipindupindu
Kipindupindu ni kuharisha papo hapo.Huu ni ugonjwa ambao unaweza kuua ndani ya masaa kama ukiachwa bila kutibiwa.
Mara tu baada ya ugonjwa kupatikana ni jambo la muhimu kutafuta matibabu ya haraka.
Utoaji au utumiaji wa maji safi,vyoo bora na elimu ya afya kwa umma na usafi wa mazingira,ni baadhi tuu ya namna ya kupunguza madhara au kukabiliana na tishio la ugonjwa wa kipindupindu.
Afya yako iko mikononi mwako.Kampeni ya kuosha mikono baada ya kwenda chuooni ni muhimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni