Jumatatu, 12 Septemba 2011

Obstetric fistula

Fistula
Katika baadhi ya mikoa hapa nchini Kenya, akina mama waja wazito hulazimika kutembea  mwendo  mrefu kutafuta matibabu.Baadhi yao  hulazimika kujifungua nyumbani ,jambo ambalo husababisha madhara ya kiafya.

Uchungu wa muda mrefu,kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu  au kujifungua katika mazingira yasiyofaa ni chanzo cha ugonjwa unaojulikana kama fistula.
Kulingana na daktari wa afya ya uzazi katika hospitali moja hapa jijini Nairobi,Fistula ni tatizo linalotokana na jeraha wanalopata kina mama wakati wa kujifungua baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu na pia kuwa na njia ndogo ya uzazi kiasi kwamba kichwa cha mtoto kinashindwa kupita kwa usalama wakati wa kujifungua.

Hali hii humfanya mama kushindwa kujizuia wakati anapotaka kwenda haja ndogo na wakati mwingine hata kubwa bila mpangilio.

Ugonjwa huu ,umehatarisha maisha ya akina mama wengi.

 
Wengi wao hutengwa na jamii kwani wanakuwa hawawezi kufanya lolote,na pia wanatoa harufu inayosambabishwa na kuvuja kwa mkojo.Hawana uwezo wakuzuia haja kubwa wala ndogo.

Takwimu za Shirika Afya Duniani (WHO) sinadhihirisha ya kuwa zaidi ya  wanawake milioni nne ulimwenguni kote wanaishi na fistula .
Daktari wanatilia mkazo  haja ya wanawake wajawazito  kutembelea kliniki za afya mara tu wanapotunga mimba ,ili kupata utalamu na mawaidha ya afya,hili kupunguza hatari.
Nchini Kenya kuna baadhi ya mashirika ya afya yaani mashirika yashiyo ya serikali ,yanayotoa matibabu ya bure kwa baadhi wa wanawake ambao wamejikuta kwenye lindi hili na masonokeko.

Jambo la kutia moyo ni kuwa tatizo hili linaweza kutatuliwa.Baadhi ya wanawake niliowahoji wanasema kuwa baada ya  upasuwaji na watalaamu wa afya ya uzazi,walirejea katika hali zao za kawaida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni