Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2020

America COVID- 19

Marekani yaongoza duniani kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimetoa takwimu kuwa   watu 85,996 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani.  Hivyo basi,    Marekani imekuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi hivyo duniani. Huku idadi ya  Vifo ikifika 1,195. Idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo imeongezeka kwa zaidi ya watu elfu kumi ndani ya saa tano nchini Marekani,inasema ripoti hiyo.   Pia Tafiti zinaonyesha   idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imefika   542,788 na 24,361 wamefariki kwa virusi hivyo duniani. Kwa sasa Marekani imeipita Uchina na Italia kwa visa vya Corona vilivyothibitishwa. Hata hivyo,bado Italia inaongoza kwa vifo 8,000 huku Uchina ikifuata na idadi ya vifo 3,000 hadi sasa. Ugonjwa wa Corona unaenea kwa kasi huku mataifa ya dunia yakijukakamua kukabiliana na hali kwa kuweka mikakati thabiti ya k...

kifua kikuu-WHO

Kifua kikuu --mikakati yabuniwa Dunia imeadhimisha siku ya kifua kikuu,huku idadi ya maambuziki ikizidi kuongezeka. Hali hii imepelekea wataalamu wa afya duniani kutafuta mikakati itakayo badili hali ili kupunguza idadi ya wagonjwa na walioko kwenye hatari ya maambukizi. Takwimu zinaonyesha kuwa robo ya watu duniani wana backeria ya kifua kifuu mwilini na wako hatarini ya maambukizi,hasa wale walio na kinga dhaifu. Kufuatia haya,Shirika la Afya Duniani,WHO limetoa mapendekezo, kuongezwa kiwango cha matibabu ya kuzuia Kifua kikuu kati ya idadi ya watu walio katika hatari kubwa. Mapendekezo hayo ni kama vile:kuboresha ubunifu kuzuia hali ya wagonjwa wa kifua kikuu, watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na pia   wanaoishi katika mazingira yaliyojaa. WHO inapendekeza kwamba ama majaribio ya tuberculin au interferon-gamma (IGRA) itumiwe kupima ugonjwa wa Kifua kikuu. Upimaji wa maambukizo ya Kifua Kikuu,ingawa hauhitajiki kabla ya kuanza tiba ya kinga kwa wat...

Kifo Corona Kenya

Picha
Kifo cha Kwanza kutokana na mambukizi ya Corona, COVID 19 cha tangazwa Kenya. Kulingana na taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe,  mwadhiriwa amefariki Leo katika hospitali ya Agah Khan alipokuwa akipokea matibabu. Idadi ya wanaougua Ugonjwa wa Corona yazidi kuongezeka, huku serikali ikitoa makataa yakutotoka nje kutoka alasiri hadi machweo kuanzia hapo kesho, Ijumaa. Zaidi ya hayo, Kenya ina maambukizi zaidi ya watu 30.

Dr Catherine Hamlin afariki

Picha
Daktari wa Afya ya akina mama ,Dkt Catherine Hamlin Amefariki Dunia huko Ethiopia akiwa na umri wa miaka 96. Dkt Hamlin ni mzaliwa wa Australia na alikuja Afrika katika shughuli za kazi ya utaalamu wa afya ya wanawake. Alijitolea kwa moyo wa dhati  kuwasidia akina mama hususan nchini Ethiopia kuwanusuru kutoka kwa ugojnwa wa fistula ambao humwacha mwanamke na fedheha. Dkt  Hamlin,alikuwa mkarimu ,mwenye upendo na huruma aliye jitolea kuhakikisha mwanamke amepata matibabu yafaayo anapopatwa na hali kushindwa kudhibiti mkojo baada ya kujifungua. Alipowasiri nchini Ehiopia hakukuwa na hospitali iliyowatibu wagonjwa wa fistula ya akina mama lakini alifanya juu chini kuhakikisha namna ya kurejesha heshima na matumaini kwa  akina mama imepatikana. Pamoja na mumewe walifanya ubunifu wa kutafuta namna tofauti za kufanya upasuaji wa wanawake waliona fistula ,ubunifu ambao unatumiwa na wataalamu wa afya ya kina mama hadi sasa. Fistula ni jinamizi linalowaghub...

Aurlus Mabele :COVID 19

Picha
Ugonjwa wa COVID-19 umepokonya dunia mwanamziki mashuhuri kutoka nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo(DRC). Papa Aurlus Mabele alifariki hiyo jana baada ya kuambukizwa virusi vya Corona . Hii ni kwa mujibu was taarifa zilizotolewa na familia ya mwenda zake. Mwanaye Liza Monet alitangaza kifo cha babake kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram alisema" baba amefariki asubuhi ya Leo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.Alikuwa mwanamziki mashuhuri wa mitindo ya Soukouss ambaye watu was Congo wamempoteza, nakupenda baba Aurlus Mabele." Hakika ugonjwa wa Corona ni tisho kubwa ambalo linahitaji hatua kali kulikabili. Mabele ni miongoni mwa watu washuhuri ambao wamepatikana na ugonjwa huu, ingawa wengi wao wamepata au wanaendelea kupata matibabu. Hatua kali zinahitajika hasa katika Bara la Afrika ambapo mambukizi yanaongezea kila kuchao. . Mkuu wa WHO Tedros ametoa changamoto kwa Afrika huku akisema kuwa ugonjwa hunaenea kwa kasi. Wakat...

WHO chanjo dhidi ya Coronavirusi

Shirika la Afya Duniani,WHO limezidua rasmi  chanjo  ya majaribio dhidi ya COVID – 19 . Hatua hii ni kufuatia ongezeko ya maambukizi na vifo duniani.   Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amewapongeza watafiti kote duniani ambao wamejumuika   pamoja ili kutaathimini majaribio haya. Dkt Ghebreyesus akisema hatua hii ni  mafanikio makubwa na kuwa kwa sasa wataalamu wa afya yanafanywa kila juhudi kuhakikisha kuwa tiba yeyote ambayo itasaidia kuokoa maisha imepatikana Amesema hata kama kuwa uwezekano wa kutofata mafanisi kutokana na majaribio madogomadogo na njia mbalimbali,tiba ya haraka inahitajika na kuna uhakika itapatikana . Zaidi ya hayo,Dkt. Ghebreyesus,ameongeza kuwa WHO na washirika wake wanaandaa utafiti katika nchi mbalimbali ambapo baadhi ya dawa hizi hazijafanyiwa majaribio zitalinganishwa . Amesema   utafiti huo mkubwa unaandaliwa kwa minajili ya kukusanya takwimu zinazohitajika il...

COVID -19 Tanzania

Kisa cha kwanza  cha virusi vya corona kimethibitisha  Arusha,Tanzania Inasemakana kuwa mgonjwa aliwasiri nchini kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kirimanjaro Mwezi wa Machi,15 mwaka huu. Mgonjwa huyu ni mwanamke raia wa Tanzania aliye na umri wa miaka 46. Aliwasiri kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda ambaye aliwasiri aliyetangazwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, ambaye aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda. Mtanzania huyo ambaye kwa sasa anapokea matibabu kwenye hospitali ta Rufaa ya Mt Meru Arusha,alitembelea nchi tofauti katika ziara yake huko Uraya. Alizuru Denmark,Sweden na Ubelgiji na kurejea nchini ,ingawa maabukizi ya Corona hayakuguduliwa alipowasiri nchini Tanzania. Baada ya muda,alianza kujihisi vibaya na kwenda hospitalini ambapo sampuli ilichukuliwa  na baadaye ikapelekwa kwa maabara ya kitaifa jiji Dar es salaam kwa uchunguzi. Kulinga na Waziri wa Afya Tanzania Ummy Mwalimu vipimo vya maabara...

Coronavirusi Ongata Rongai

Wakenya wamepokea tangazo  la mlipuko was virusi Corona cha Kwanza mtaani Ongata Rongai, Jimbo la Kajiado kwa hofu . Kufuatia hali hii Wakenya wengi hasa wa Ongata Rongai wamebakia nyumbani hii wikendi  wakihofia maambukizi. Maadhi ya shule na pia vyuo vikuu vimetoa taarifa kuwataka wanafunzi kubaki nyumbani, hadi Hali iwe sawa. Jumapili kama kawaida kanisa huwa zimefurika lakini Hali imekuwa tofauti. Wengi wameamua kufanya maombi nyumbani yote haya yakiwa kuepuka maambukizi ya virusi vya Covid 19. Ugonjwa huu uenea kwa kasi kwenye mataifa tofauti ulimwenguni.

Corona Virusi Kenya

Kenya yathibithisha kisa cha kwanza Corona siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani kutangaza mlipuko huu kama janga la kimataifa. Hii imetangazwa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe. Waziri alisema virusi hivyo vilitibitishwa kwa mwafunzi wa kike,mkenya ambaye alisafiri kutoka marekani kupitia Uingereza. hata hivyo mgonjwa huyo yuko katika hali nzuri ingawa atatibitiwa hadi pale hali yake ya afya itathibitiwa kikamilifu. ·           Waziri amesema ni jukumu ya kila mtu kuchukua tahadhari ilikuepuka maambukizi ·           Kunawa mikono mara kwa mara. ·           Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya - simama umbali wa mita moja ·           Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi ·      ...

WHO Corona janga

Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mkulupuko was virusi ya Corona kama janga la kimataifa. Mkurugenzi wa WHO Dkt Tedros amesema viwango vya maambukizi vimeenea katika maeneo mengi nje ya nchi ya Uchina kwa mara 13. Tangazo hili limetolewa huku nchi ya Italiano ikiwa na idadi kubwa ya maambukizi baada ya Uchina. Dkt Tedros anasema kuwa "ana hofu kubwa " kutokana na "viwango vya maambukizi " ya virusi. Hata hivyo, Dkt Tedros ameongeza kuwa kuuita ugonjwa janga haimaanishi kuwa WHO  inabadilisha ushauri wake juu ya kile mataifa yanapaswa kufanya. Ametowa wito kwa serikali kubadili jinsi zinavyo shughulikia mlipuko kwa kuchukua hatua za dharura. "Nchi kadhaa zimeonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kudhibitiwa ,"amesema. Virusi vya Corona vilidhihirika mwishoni mwa mwaka jana wa 2019 katika mji wa Wuhan mkoani Hubei mashariki mwa China; na hadi sasa  virusi hivyo vimeenea katika nchi zaidi ya 119 ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, Asu...