Alhamisi, 19 Machi 2020

Aurlus Mabele :COVID 19

Image result for aurlus mabele pix
Ugonjwa wa COVID-19 umepokonya dunia mwanamziki mashuhuri kutoka nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo(DRC).

Papa Aurlus Mabele alifariki hiyo jana baada ya kuambukizwa virusi vya Corona .

Hii ni kwa mujibu was taarifa zilizotolewa na familia ya mwenda zake.

Mwanaye Liza Monet alitangaza kifo cha babake kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram alisema" baba amefariki asubuhi ya Leo kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.Alikuwa mwanamziki mashuhuri wa mitindo ya Soukouss ambaye watu was Congo wamempoteza, nakupenda baba Aurlus Mabele."

Hakika ugonjwa wa Corona ni tisho kubwa ambalo linahitaji hatua kali kulikabili.

Mabele ni miongoni mwa watu washuhuri ambao wamepatikana na ugonjwa huu, ingawa wengi wao wamepata au wanaendelea kupata matibabu.

Hatua kali zinahitajika hasa katika Bara la Afrika ambapo mambukizi yanaongezea kila kuchao.
.
Mkuu wa WHO Tedros ametoa changamoto kwa Afrika huku akisema kuwa ugonjwa hunaenea kwa kasi.

Wakati huo huo WHO iko katika harakati ya kutafiti chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Corona ambao kwa hakika unaogovya.

Huku dunia ikihofia maafa zaidi,ni matumaini ya kila mmoja Kuwa shuluhu la dharura litapatikana kukabiliana na janga hili,  ili kuepuka maafa zaidi.

Kampeni pia zinahitajika ili kuwahamasisha wananchi madhara yake na jinsi ya kuepuka mambukizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni