Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mkulupuko was virusi ya Corona kama janga la kimataifa.
Mkurugenzi wa WHO Dkt Tedros amesema viwango vya maambukizi vimeenea katika maeneo mengi nje ya nchi ya Uchina kwa mara 13.
Tangazo hili limetolewa huku nchi ya Italiano ikiwa na idadi kubwa ya maambukizi baada ya Uchina.
Dkt Tedros anasema kuwa "ana hofu kubwa " kutokana na "viwango vya maambukizi " ya virusi.
Hata hivyo, Dkt Tedros ameongeza kuwa kuuita ugonjwa janga haimaanishi kuwa WHO
inabadilisha ushauri wake juu ya kile mataifa yanapaswa kufanya.
Ametowa wito kwa serikali kubadili jinsi
zinavyo shughulikia mlipuko kwa kuchukua hatua za dharura.
"Nchi kadhaa zimeonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kudhibitiwa
,"amesema.
Virusi vya Corona vilidhihirika mwishoni mwa mwaka
jana wa 2019 katika mji wa Wuhan mkoani Hubei mashariki mwa China; na hadi
sasa virusi hivyo vimeenea katika nchi zaidi ya 119 ikiwa ni pamoja na
Marekani, Uingereza, Asutralia,Thailand, Korea ya Kusini, Japan, Canada,
Ufaransa, Italia, Iran, Saudi Arabia na Imarati licha ya
kuiathiri mikoa 30 ya China.
Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia sasa watu
wasiopungua 119,000 wameambukizwa virusi vya corona duniani.
Watu 66,000
miongoni mwao wamepona na zaidi ya elfu nne wameaga dunia kwa maradhi
hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni