Marekani yaongoza duniani kwa
idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona
Chuo Kikuu cha Johns
Hopkins kimetoa takwimu kuwa watu 85,996 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani.
Hivyo basi, Marekani imekuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi hivyo duniani.Huku idadi ya Vifo ikifika 1,195.
Hivyo basi, Marekani imekuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi hivyo duniani.Huku idadi ya Vifo ikifika 1,195.
Pia Tafiti zinaonyesha idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa
virusi vya Corona imefika 542,788 na 24,361 wamefariki kwa virusi hivyo duniani.
Hata hivyo,bado Italia
inaongoza kwa vifo 8,000 huku Uchina ikifuata na idadi ya vifo 3,000 hadi sasa.
Ugonjwa wa Corona unaenea
kwa kasi huku mataifa ya dunia yakijukakamua kukabiliana na hali kwa kuweka
mikakati thabiti ya kukomesha maamukizi Zaidi.
Hiyo jana Kenya ilirekodi
kifo cha kwanza cha mgonjwa aliyekuwa akipokea matibabu kwa muda.
Mkenya huyo wa miaka 66
alikuwa amezuru nchi ya uswatini Afrika kusini .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni