Shirika la Afya Duniani,WHO limezidua rasmi chanjo ya majaribio dhidi ya COVID – 19 .
Hatua hii ni kufuatia ongezeko ya
maambukizi na vifo duniani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus
amewapongeza watafiti kote duniani ambao wamejumuika pamoja ili kutaathimini majaribio haya.
Dkt
Ghebreyesus akisema hatua hii ni mafanikio makubwa na kuwa kwa sasa wataalamu wa
afya yanafanywa kila juhudi kuhakikisha kuwa tiba yeyote ambayo itasaidia
kuokoa maisha imepatikana
Amesema hata
kama kuwa uwezekano wa kutofata mafanisi kutokana na majaribio madogomadogo na
njia mbalimbali,tiba ya haraka inahitajika na kuna uhakika itapatikana .
Zaidi ya hayo,Dkt. Ghebreyesus,ameongeza
kuwa WHO na washirika wake wanaandaa utafiti katika nchi mbalimbali ambapo
baadhi ya dawa hizi hazijafanyiwa majaribio zitalinganishwa .
Amesema utafiti huo mkubwa unaandaliwa kwa minajili ya
kukusanya takwimu zinazohitajika ili kubainisha ni matibabu yapi yanafayakazi
zaidi.
Licha ya hayo, nchi kadhaa tayari
zimethibitisha kwamba zitashiriki utafiti huo wa Mshikamano wa majaribio.
Nchi hizo ni
kama vile, Argentina, Bahrain, Canada, Ufaransa, Iran,
Norway, Afrika Kusini, Hispania, Uswisi na Thailand.
Kuna matumaini kuwa nchi zingine
ulimwenguni zitajiunga ili kuhakikisha jawabu au tiba ya COVID -19 imepatikana.Jambo
ambalo WHO imelichangamkiakwani linatia moyo
Dkt. Tedros anasema kuwa hatua za mshikamano
dhidi ya COVID-19 kumepelekea mchango wa zaidi ya dola milioni 43 kutoka kwa
watu zaidi ya 173,000 na mashirika hisani siku chache tu tangu ulipozinduliwa.
FIFA ni
baadhi ya mashirika ambayo yamechangia mfuko huu kwa kutoa dola milioni 10.
Utafiti
huo umepewa jina la “Majaribio
ya mshikamano”.
Amesisitiza kwamba virusi hivi ni tishio
kubwa lakini kwa pamoja litakabiliwa.Isitoshe, WHO imesema kuna hofu jinsi Bara
la Afrika linavyochukulia janga hili.
Hapo awali takwimu zilionyesha
maambukizi yalikuwa kiwango za chini barani Afrika lakini mambo yamebadilika kwa
kasi huku idadi ya maambykizi ya kuongezeka.
Ametaka serikali za Afrika kuchukua
janga hili kwa dharula ili kulikabili.
Taharuki imetanda nchi DRC baada ya visa 600 kuripotiwa.
serikali ya Congo imejitahidi kukabiliana na hali hii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni