Kifua kikuu --mikakati yabuniwa
Dunia imeadhimisha siku ya kifua kikuu,huku idadi ya
maambuziki ikizidi kuongezeka.
Hali hii imepelekea wataalamu wa afya duniani kutafuta
mikakati itakayo badili hali ili kupunguza idadi ya wagonjwa na walioko kwenye
hatari ya maambukizi.
Takwimu zinaonyesha kuwa robo ya watu duniani wana backeria
ya kifua kifuu mwilini na wako hatarini ya maambukizi,hasa wale walio na kinga
dhaifu.
Kufuatia haya,Shirika la Afya Duniani,WHO limetoa
mapendekezo, kuongezwa kiwango cha matibabu ya kuzuia Kifua kikuu kati ya idadi
ya watu walio katika hatari kubwa.
Mapendekezo hayo ni kama vile:kuboresha ubunifu kuzuia hali
ya wagonjwa wa kifua kikuu, watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na pia wanaoishi katika mazingira yaliyojaa.
WHO inapendekeza kwamba ama majaribio ya tuberculin au interferon-gamma
(IGRA) itumiwe kupima ugonjwa wa Kifua kikuu.
Upimaji wa maambukizo ya Kifua Kikuu,ingawa hauhitajiki kabla
ya kuanza tiba ya kinga kwa watu wanaoishi na VVU, na watoto chini ya miaka 5.
Pia ,WHO inapendekeza mbinu fupi, jinsi ya kutumia dawa
kukabili TB kwa kupunguza muda wa awali wa miezi 6 .
Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa
maabukizi,mllioni 10 na vifo vya
takribani watu million 1.5 duniani mwaka wa 2018.
Juhudi hizi zinafanywa wakati dunia ikikabiliana na
jinamizi la Virusi vya Corona huku Mkuu wa WHO Tedro Ghebreyesus akissitiza
umuhimu wa kuendele na juhudi za kukabiliana na magonjwa haya yakuambukiza,ili
kuokoa maisha.
Ingawa maendeleo yamepatikana kwenye malengo yaliowekwa
kupunguza makali ya TB juhudi za nchi wanachama zahitajika zaidi ilikuafikia
malengo ya kukomesha Tb ifikiapo mwaka wa 2030.
Kenya yajizatiti kuhakikisha wanaougua Tb wanapokea
matibabu na pia lishe bora ili kuimalisha afya na idadi ya maambukizi.
Hata hiyo juhudi zaidi hasa mashinani zinahitajika.juhudi
za kuelimisha umma na namna ya kupata matibabu iendelezwe kwa kina.
Mwaka jana Wizara ya Afya kenya ilizidua mwongozo na malengo yakupunguza maambukizi ya watu 597,000
ifikapo mwaka wa 2023
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni