Kenya
yathibithisha kisa cha kwanza Corona siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani
kutangaza mlipuko huu kama janga la kimataifa.
Hii imetangazwa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.
Waziri alisema virusi hivyo vilitibitishwa kwa mwafunzi wa kike,mkenya ambaye alisafiri kutoka marekani kupitia Uingereza.
hata hivyo mgonjwa huyo yuko katika hali nzuri ingawa atatibitiwa hadi pale hali yake ya afya itathibitiwa kikamilifu.
- · Waziri amesema ni jukumu ya kila mtu kuchukua tahadhari ilikuepuka maambukizi
- · Kunawa mikono mara kwa mara.
- · Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya - simama umbali wa mita moja
- · Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi
- · ametakiwa kusalia nyumbani.
- · marufuku yotolewa kwa mikutano ya aina yote ikiwemo ile ya umma kama vile ya kidini, michezo, na wanaotaka kwenda ya watu
- · Hakikisha kwamba unaziba pua na mdomo unapokohoa kwa kutumia kitambaa ama tishu.
- · Mtu anayehisi joto ama tatizo la kupumua makanisani na msikitini watalazimika kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia katika sehemu hizo.
- · Michezo yote ya shule imepigwa marufuku ingawa shule zote zitasalia wazi kwa wakati huu.
- · Wachukuzi wa umma wametakiwa kuhakikisha kuwa abiria wanaosha mikono yao kabla ya kuabiri magari hayo.
- · Wakenya kuto toka nje ya nchi isipokuwa wale wenye umuhimu mkubwa wa kusafiri .Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuelekea katika mataifa yenye visa vingi vya ugonjwa huo.
- · Serikali imedokeza kwamba itatoa maelezo kuhusu ugonjwa huo kila siku,na kuwataka wakenya kutoeneza habari za uongo za viruzi vya Covid 19 Corona
Hapo
wali serikali ya kenya ilitenga vyumba maalum vya kuwatibia wanaopatikana na
virusi vya Corona katika hospitali ya Mbagathi.
Virusi va Corona hafibagui yeyote kwani kwa siku za hivi karibuni watu mashuhuri duniani wameambukizwa.
Wanasiasa
,wanamichezo na waigizaji maarufu ni miongoni mwa waadhirika.
Pia
Waziri wa Afya wa Uingereza ,Nadine Dorries ameambukizwa Corona.
Mke
wa Waziri Mkuu wa Canada Bi Sophie Tredeau anakisiwa kuambukizwa Virusi vya
Corona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni