Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2014

Dr Umar Khan afariki

Daktari mashuhuri wa ebola amefariki. Dk. Sheik Umar Khan   Alijitolea  mhanga kuwatibu  walio ambukizwa  Virusi vya ebola. Hata hivyo ajari haina kinga katika harakati ya kuhakikisha kuwa amewatibu wagonjwa, alipata Virusi vya ebola wiki moja iliyopita. Hivi majuzi kwenye mahojiano na wana Habari, Dk.Umar alisema yeye kama mwanadamu yeyote anathamini uhai na alihofia uhai wake lakini hangeacha kutekelezwa wajibu wake. Mola ailaze roho yake mahali pema peponi. Idadi ya vifo nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia Inakisiwa kuwa 672 kutoka Februali mwaka huu.

cancer conference,windhoek

Picha
                                        Kongamano la saratani  Mkutano kuhusu ugonjwa hatari wa saratani umeanza hii leo  mjini Windhoek,Namibia. Mkutano huu hulifunguliwa na rais Hifikepunye Pohamba huku akisema ni muhimu kwa umoja wa Afrika na pia mataifa tofauti Afrika kutafuta binu na mikakati ya kuangamisha saratani. Mada ya mkutano huu ni kuendelea na mikakati ya kutambua na kutibu   saratani ya shingo ya uzazi yaani cervical cancer  imekuwa donda ndungu kwa wanawake .Saratani ya matiti pia inaenea kwa haraka barani Afrika. Malengo mengine ni kutafuta binu ya kuzuia  kenea kwa saratani ya shingo ya uzazi ifikapo mwaka wa 2030. Rais Pohamba alilalama kuwa zaidi ya watu millioni  28 hufariki kutokana na maradhi ya saratani kila mwaka jambo...

AIDs conference

Picha
Kongamano la kimataifa  kuhusu  ukimwi latia nanga  ,huku washiriki wakitoa heshima kwa wenzao waliofariki kwenye ajari ya ndege ya Malaysia.  Husuni ilitanda kote kwenye ukumbi huyo wa mikutano. Hakika kifo cha wataalamu hao sita  ni pigo kwenye kongamano hilo na ulimwengu kwa jumla. Aliwataja kama mashujaa na watafiti  yalihobea katika nyanja ya utafiti na afya. Rais wa Shirika la Ukimwi Duniani, Francoise Barre-Sinoussi alisema hata baada ya mkasa huo washiriki wataendelea kufanya vikao wakiwa na lengo la  kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi.  Shirika la Afya Duniani(WHO) pia limepata pigo baada ya msemaji wake Glenn Thomas ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mwadishi wa Shirika la Utangazaji la BBC . Glenn raia wa uingereza alipenda sana kuangazia maswala ya afya na alitumika katika shirika la WHO kwa miaka kuni.Kwa hakika viti vyao vilibaki wazi huku  vitambulisho vyao vikibaki mezani huku  majukumu waliotengewa ka...

Aids2014..ukimwi melbourne

Picha
                                         MKUTANO KUHUSU UKIMWI 20                                           Mkutano unatarajiwa kuanza jumapili mjini Melbourne, Australia.watalaamu wa afya na watafiti wa makali ya ukimwi duniani kote wamealikwa.    Habari njema ni kuwa maambukizi ya ukimwi imepunguka kote ulimwenguni . Shirika la Ukimwi duniani linabaini   kuwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na ukimwi duniani vimepungua kwa kasi mwaka 2013 sawa na asilimia 11.8% ndani ya mwaka mmoja. Zaidi ya hayo UNAIDS inasema kwamba lengo l...

Joep Lange

Picha
Jeop Lange mtafiti wa tiba ya makali ya ukimwi aaga dunia. -Sekta ya afya na tiba, na dunia kwa jumla inaomboleza kifo za Jeop Lange, mtafiti wa tiba ya makali ya ukimwi dunia. Mtafiti stadi wa afya duniani ni miongoni mwa  abiria waliofariki baada ya ndege ya Malaysia,waliokuwa wakisafiria, kuanguka huko Ukraine. Joep Lange alikuwa mwanasayansi mashuhuri ambaye pamoja na watafiti wenzake lifanya juu chini kutafuta tiba ya ugonjwa wa ukimwi duniani.  Lange Pia ni raia wa Uhoranzi. Lange alikuwa profesa na mkurugenzi kuu wa kitengo cha afya na utabibu katika chuo kikuu cha Amsterdam,uholanzi.Amekuwa katika mstari wa mbele kutafuta tiba ya makali  ya ukimwi kwa miaka thelathini.Mkewe pia alifariki kwenye ajari hiyo. Mtafiti kutoka Amerika,Dkt Rick Elion alimtaja Lange kama mtu mwenye roho ya dhahabu,mkarimu na mwenye bidii kama ya mchwa. Inakisiwa baadhi ya  abiria kwenye ndege hiyo  ya Malaysia  walikuwa wataalamu wa afya na watafiti ...

fistula Kenyatta National Hospital

Picha
Ugonjwa wa fistula umekuwa ni kero kwa akina mama wanaokubwa na hali hii.  Habari njema ni Kwamba wanaougua fistula sasa wana sababu ya kutabasamu. Hospitality kuu ya kitaifa ya Kenyatta kwa ushirikiano na wadau wengine katika sekta ya afya wametangaza kuwa kuanzia tarehe 4-18 Julai mwaka Huu watatoa matibabu ya bure kwa wote. Huduma hii inatolewa bila malipo ilikumrudishia hadhi mwanamke anaye baguliwa, kukejeliwa na kuteswa na jamii kufuatia Hali yake. Baadhi ya akinaHabari mama ambao wamefaidika kupitia Huduma hii wanasema wamezaliwa upya na wanasababu  ya kuishi tena. Kuna wengine ambao wamejiua kufuatia unyanyapa na kutekelezwa na jamii. je fistula ni nini? Tundu kwenye mango was uzazi.  Tundu hili linaweza kutokea kati ya uke na njia ya haja kubwa au kati ya kibofu na uke baada ya mama kushindwa kujifungua au kutumia muda mrefu kujifungua. Pia kunajisiwa kunaweza kusababisha hali hii.Matokeo yake ni kwamba wanawake wenye fistula hujikuta katika matatiz...

siku ya saratani duniani

Picha
  Wanasayansi wanaamini kuwa unywaji mwingi wa pombe unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida mwilini ambazo zinaweza kuiweka ngozi katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya ngozi. Kemikali ya Ethanol inapogeuzwa kuwa “Acetaldehyde” baada ya ulaji wa chakula,kemikali hii yaweza kuiwezesha ngozi kupenyeza miale hata ya jua (UV light) Taarifa zinazohusiana Watafiti waliofanya ugunduzi huo, nchini Uingereza wanakubali kwamba kuna mambo mengine yanayochangia mtu kupata Saratani ya Ngozi. ''Utafiti umeonyesha kuwa wagonjwa wanaougua Melanoma huathirika kwa ajili ya kuota jua kwa muda mrefu,hili linaweza kupunguzwa iwapo mtu atajikinga kutokana na jua kali,'' asema Sarah Williams wa Utafiti wa Kansa, Uingereza. Kulingana na utafiti wao uliochunguza mada 16 tofauti na kushirikisha maelfu ya watu,unywaji wa chupa moja ya pombe moja au zaidi ...

cancer day

Picha
  leo ni siku ya ugonjwa wa saratani duniani   Uraibu wa pombe na sigara husababisha saratani   Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa saratani kote duniani. Shirika hilo limesema nusu ya ugonnjwa wa Saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili kufanyika ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi, ulevi na uvutaji sigara. Watu milioni kumi na nne wanajulishwa kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha miongo miwili ijayo. Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa Saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu.   Taasisi hiyo imesema serikali zinahitajika kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu matumiz...

Anne Waithera Aaga dunia (BBC)

Picha
Saratani Saratani...saratani nenda zako ...tuachie afya zetu!!! Mwandishi wa Shirika la utangazaji la Uingereza ( BBC) Anne Waithera Ameaga dunia. Hii leo nina husuni tele ninapoandika kuhusu kifo cha rafiki na wandishi menzangu Anne Waithera. Waithera alikuwa mtangazanji katika shirika la utangazaji la BBC ambaye pia alipenda sana kuandika kuhusu maswala ya afya. Ann amekuwa akiugua saratani. Katika enzi za uhai wake alifanya kazi na kituo cha habari cha Royal Media Services Citize,Nation Media Group.  Aliwahikutunukiwa zawadi katika nyanja ya afya na mazingira na mashirika tofauti ikiwemo Internews. Mola ailaze roho yake mahari pema peponi.

Jerry Okungu afariki

Picha
Ugonjwa hatari wa saratani umetupokonya mwandishi mashuhuriJerry Okungu. Okungu  alifariki  katika hospitali ya MP Shah,Nairobi alipokuwa akipokea matibabu. Alikuwa akiugua saratani ya tezi kibofu, . Mola ailaze roho yake mahari pema peponi.