Jumatano, 13 Novemba 2019

kongamano laicpd 25



Uhuru Kenyatta welcomes delegates at the Summit's opening. © Nairobi Summit


Rais uhuru Kenyatta afungua rasmi Kongamano la idadi ya watu na maendeleo ICPD25 jiji Nairobi .
Rais amehakikisha kuwa serikali ya Kenya itaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa swala la ukeketaji wa wanawake limekabiliwa .

Pia ametaka mataifa menginekuhakikisha haki za wanawake na jamii zinaheshimiwa.
Upashaji tohara nchi na pia barani Afrika imekuwa ikiendelea licha ya hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika.

Kulingana na tafiti wanawake waliopashwa tohara wanakuwa  hatarini wanapojifungua huku wengine wakifariki wakati wa kujifungua.


ICPD 25 NAIROBI



Image result for https://www.nairobisummit demo
Kongamana kuu la kimataifa limengoa nanga  nchini Kenya huku maswala ya afya ya uzazi yakiorodheshwa kuwa kipaombele kati ya maswala nyeti yatakayo jadiliwa.

Isistoshe,malengo makuu tano yanayolengwa katika mjadala wa siku tatu wa kongamano la (ICPD25) ni kama vile ; haki ya afya ya uzazi,dhuluma za kijinsia na tabia tofauti ambazo zinaadhiri wanawake.

Hata hivyo kuna baadhi ya vikundi ambavyo vina tofautiana na mkutano huu, hususan kuhusu maswala  ya uaviaji mimba na ngono za jinsia sawa yaani ushoga na ushagaji.

Mashirika ya kidini yalipinga kuwa endapo maswala haya yatapewa nafasi ya kwanza, hawatahudhuria,huku wakisisitiza kuwa yanapinzana na desturi na mwelekeo wa dini.
Vingozi wa dini wanakashifu hatua ya mkutano huu kwa kusema kuwa uaviaji mimba ni kitendo ambacho ni dhambi na pia ushoga hauna nafasi katika dini .

Kwa mfano kanisa katoliki duniani hawaruhusu matumizi ya aina yeyote ya uzazi mpango hospitali wanazomiliki na zsisitiza ni dhambi.

Mwaka jana kasisi mmoja alikata kufanya maombi ya wafu kwa mama aliyefariki na aliyedaiwa kuavya mimba.

Hata ikiwa  maswala haya yanajitokeza wakati wa mkutano huu,hakika ni kuwa kuna sababu za kiafya ambazo muunguzi anaweza kumshauri mgonjwa kuavya mimba endapo maisha yake yatakuwa kwenye hatari.

Hata hivyo mkutano uliendelea kama kawaida huku kukiwa na lengo la kurai serikali kuchangia kueneza malengo haya kifedha na pia kisiasa.

Takwimu zilizotolewa zinaonyesha kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi sita ambazo zinaendelea kushamili katika maswala ya uzazi mpango, huku idadi ya wanaotumia njia za kisasa za uzazi mpango ikiongezeka.

 Ripoti iliyozinduliwa mkabala na mkutano huu inaonyesha kuwa Kenya imepiga hatua kukumbatia matumizi ya kondomu,sindano na vidonge.

Mkutano huu umeadaliwa na shirika la idadi ya watu na serikali za Kenya na Denmark .
Mkutano kama huu ulifanyika Zaidi ya miaka ishirini huko Cairo,Misri ambako azimio la Cairo lililatibiwa.



Jumanne, 24 Septemba 2019

WHO -UHC (universal health Coverage)


Azimio la afya kwa wote

Image result for universal health coverage new yorkSekta ya afya duniani imepata mafanikio  mwafaka baada ya Viongozi wa ulimwengu kupitisha rasmi Azimio la Kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu afya kwa wote  (UHC) ifikapo mwaka wa 2030.
Kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu afya kwa wote, katika Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa jijini New york, Marekani ,Viongozi walitoa hoja kuwa ni muhimu swala la afya kwa wote lishighulikiwe kwa haraka na wakaridhia lipitishwe rasmi na baraza kuu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutumu kwenye kikao hicho alisema,ingawa afya ni haki ya kila mtu, bado nusu ya watu ulimwenguni  wanakosa haki yao ya msingi.

Image result for president kenyatta meets guterres in new york Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema kuwa hii ni hatua muhimu na ni jukumu ya mataifa husika kuhakikisha malengo haya yameafikiwa ifikapo mwaka wa 2030.

Dk Ghebreyesus akisema Ulimwengu umebakisha miaka 11 kuyatekeleza majukumu haya mwafaka ya afya.

Aliwapongeza viongozi kwa kuchukua uamuzi wa kisiasa wa afya kwa wote.

Azimio hilo linakuja siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wake kuweka mikakati ya kuboresha kwa mara mbili viwango vya afya  kabla ya mwaka 2030 ili kuhakikisha  watu bilioni 5 wasioweza kupata huduma ya afya hawaja achwa nyuma kwenye mpango huu.
Image result for rural kenya health facility
Hii ni  kuwa haya yakizingatiwa, hakuna mtu atapata ugumu wa kupata matibabu ya afya kwa kukosa pesa za kugharamia matibabu.

Pia serikali zinatarajiwa kutekeleza mipango ya kiafya yenye athari kubwa kupambana na magonjwa na kulinda afya ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Bill & Melinda Gates, Melinda Gates ambaye ni mfadhili mkuu kwenye sekta ya afya alisema huu ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii ili  kubadili ahadi hizo kuwa matokeo.

Wafadhili na serikali za nchi zinahitaji kusonga mbele zaidi kama kawaida ili kusaidia mifumo ya huduma ya afya inayoshughulikia mahitaji mengi ya watu kwa maisha yao yote, "alisema Gates.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliohudhuria kikao hiki.
Hapo awali,rais Kenyatta alikutana na Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Kenya ni mojawapo ya nchini inayofanya bidii kuhakikisha afya ya wote imepewa kibao mbele.

La muhimu ni kuhakikisha maswala ya afya yametekelezwa ili kupunguza idadi ya yaafa yanayokokea kutokana na ukosefu wa huduma za afya.

Mnamo tarehe 24 Septemba, WHO na mashirika mengine 11 ya kimataifa, ambayo kwa pamoja huchangia kwa  theluthi moja ya msaada wa maendeleo kwa afya, itazindua Mpango wao wa Global Action wa afya na ustawi kwa wote na kufikia malengo yanayohusiana na afya ya SDG.

Viongozi wa dunia  wataripoti juu ya maendeleo yao kwa Mkutano Mkuu wa U.N. mnamo 2023.




Ijumaa, 13 Septemba 2019

chanjo ya malaria


Jaribio la chanjo ya malaria

Huku ugonjwa wa malaria ukiwa miongoni mwa magonjwa hatari duniani,mbinu za kuukabili ugonjwa huu zinaendelea kuguduliwa kila uchao.

Hii leo,nchi ya  Kenya itakuwa miongoni mwa nchi tatu barani Afrika zinazozindua majaribio ya chanjo ya kwanza ulimwenguni dhidi ya malaria.

Nchi zingine kuzindua na kushiriki  katika mpango huu ni Ghana na Malawi.

Zaidi ya watoto 300,000 chini ya miaka miwili wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo kila mwaka Katika nchi zote tatu.

Chanjo hiyo inayofahamika kama RTS,S ina mchanganyiko wa dawa inayoisaidia mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na mbu wanaosababisha malaria.

Hapo awali majaribio madogo yalionyesha kuwa karibu watoto wanne kati ya 10 kati ya umri wa miaka mitano na 17, waliopata dozi zote nne za chanjo hiyo, walilindwa.
Chanjo hii imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 30.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema hii inaweza kubadilika mchezo, lakini inasema chanjo hiyo inatakiwa kutumika kwa mbadala na viandarua na pia dawa .
Malaria inaua watu zaidi ya 400,000 kwa mwaka - zaidi ya nusu yao wakiwa  watoto kutoka Afrika ,Jangwa la Sahara.

Waziri wa Afya wa Kenya Bi Cecily kariuki ataongoza taifa kuzidua mpango huu katika jimbo la Homabay.Serikali imesema kuwa mpango huo utajumuishwa katika mpango wa kitaifa wa chanjo.Huku watoto wa umri wa miaka (6)sita,saba (7) na tisa (9)na miezi 24 wakipata chanjo

Majimbo ya Kisumu,Migori,Bungoma,Busia,Siaya,Vihiga,Kakamenga na mombasa yatafaidika katika mpango huu.

Ingawa serikali imechua hatua kukabili malaria ,bado changamoto ziko.
Hivi mrupuku wa malaria uliua watu wanane Baringo.

Malaria huenezwa na kuumwa na mbu aina ya Anofelesi.

Watoto wa umri wa chini ya miaka 5 wako katika hatari zaidi ya kupata malaria.

Dalili za Malaria

homa kali,
kuhara,
kutapika,
kuumwa kichwa,
Kutetemeka na kuumwa mwili mzima.


Alhamisi, 29 Agosti 2019

Augmentin bandia

Image result for augmentin
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya dhidi ya matumizi ya dawa bandia ijulikanayo kama  Augmentin,nchini Kenya na Uganda.
Shirika hilo limetoa tahadhari wakati kukiwa na ongezeko la ununuzi wa dawa bila ushauri wa wataalam wa afya nchini Kenya.
 WHO imewataka wakenya wawe waangalifu dhidi ya dawa hiyo bandia ya (antibiotic) inayoamikika kuuziwa wagonjwa katika sehemu mbalimbali za nchi.
Augmentin,ni dawa ambayo hutumika dhidi ya maambukizi ya vidudu mwilini na imeorodheshwa na WHO kama mojawapo ya dawa muhimi na inapatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
Kwenye taarifa yake kwa umma, WHO imesema dawa bandia ina muonekano unaokaribiana sana na dawa halisi inayotengenezwa na kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline (GSK).
Dawa hizo bandia zilibainika baada ya  utafiti wa kukagua ubora wa dawa za antibiotic zinazouzwa kwa wagonjwa.
Baada ya vipimo kwenye maabara za kudhibiti ubora ilibainika kuwa baadhi ya dawa ya Augumentin hazikuwa na viungo muhimu vinavyohitajika na vilivyo kwemye mifuko yake ya upakiaji na pia mandishi.
Dawa bandia zinaweza kusababisha madhara makubwa mwilini,ingawa hadi kwa sasa hakuna aliyeipoti hayo,ingawa kuna wale wanaweza kuwa wameona mabadiliko wanapotumia dawa hii nawasijue ni madhara ya dawa bandia.
Serikali ya Kenya kwa muda mrefu imewaonya wananchi dhidi ya kununua dawa kwa maduka ya dawa bila kibali za daktari.Pia kuna maduka ya madawa yaliyopigwa marufuku kwa kuuza madawa bila lesheni,huku ikiaminika huwa wanauza dawa bila ujuzi elimu  unaostahili kutekeleza majukumu haya.
Hii ni mara ya mbili tahadhari dhidi ya dawa hii kutolewa na WHO barani Afrika.
Tahadhari ya kwanza juu ya uwepo wa dawa hizo bandia ilitolewa mwanzoni wa mwaka huu 2019.
Kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline imesema haihusiki kwenye utengenezaji wa   dawa hizo bandia

Jumatano, 7 Agosti 2019

breastfeeding week


Huku dunia ikiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto kuna changamoto kibao ambazo zinazokumba akina mama katika shughuli za kuhakikisha mtoto amenyonya.

Itafahamika kuwa maziwa ya mama yana faida kwa kukua kwa mtoto ikwemo umarishaji wa akili katika maendeleo ya mtoto pia inalinda mtoto dhidi ya magojwa.

Aidha,inalinda akina mama wanaonyonyesha dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi na matiti.
Image result for breastfeed africaKatika miji ilioendelea watoto hawanyonyeshwi kulingana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) linalosizitisha kuwa mtoto anastahili kunyonyeshwa  kutoka saa moja anapozaliwa hadi anapofikisha miezi sita.Watoto wa umri huu wanategemea maziwa ya mama pekee.
Hali ni tofauti kwa kiwango cha juu katika maeneo ya mashambani,kwani akina mama wanaoishi maeneo hayo  wanajikakamua kuhakikisha watoto wangenyonyeshwa kikamilifu.
Zaidi ya hayo, shirika la WHO linasema kuwa zaidi ya maisha ya watoto 800 000 walio na umri wa chini ya miaka 5 yanaweza kunusurika kila mwaka, endapo wangenyonyeshwa inavyostahili.

Pia inakadiliwa kuwa kunyonyesha mfurulizo kunaepusha vifo vya wanawake wajawazito 20,000 wanaofariki kutokana na saratani ya titi.

Kulingana na shirika la UNICEF,karibu asili mia watoto 60 hawanyonyeshwi katika miezi sita ya mwanzo iliyopendekezwa na WHO.

Changamoto

·         Kutotenga  seheme za kunyonyesha katika maeneo ya kazi
·         Likizo kwa akina mama wanaonyonyesha na walioajiriwa hazipo.
·         Ukosefu wa lishe bora na kadhalika.

Hata hivyo nchicni Kenya hali inaripotiwa kuimarika ,huku wanawake wengi wakinyonyesha watoto wao kama inavyopendekewa na WHO. 

Kadhalika ,mikakati imewekwa kuhakikisha elimu ya unyonyeshaji imefika kwenye vituo vya huduma ya afya kote nchini.

Jumanne, 6 Agosti 2019

Dkt. Sobbie Mulindi aaga dunia


Dkt. Sobbie Mulindi
Saratani imepokonya nchi ya Kenya Mtafiti wa Virusi Vya Ukimwi na mhadhiri mwandamizi katika idara ya magonjwa ya akili ya Chuo Kikuu cha Nairobi,Dkt Sobbie Mulindi.

Hadi kifo chake hiyo jana,Dkt. Mulindi alikuwa mashuhuri katika janja ya afya.

Ustadi na ukakamavu wake wa utafiti na elimu ya kupunguza maambukizi ya VVU/IKIMWI ulijulikana sio Kenya tu lakini Afrika na dunia yote kwa jumla.

 Pia Mulindi alikuwa Naibu Mkurugenzi wa zamani wa Baraza la Udhibiti wa Ukimwi la Taifa (2008-2014)
Dk Sobbie Z. A. Mulindi alianza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Nairobi, na baadaya akawa mkufunzi kwenye chuo hiko.

Zaidi ya hayo,alitumika katika hospitali kuu ya Kenyatta na katika Hospitali ya wagonjwa wa kiakili ya Mathari kufuatia uzoefu kwake katika nyanja ya wagonjwa na kiakili yaani maswala ya kisaikolojia.

Amekuwa mhadhiri katika chuo cha Nairobi kwa zaidi ya miaka 30

Isitoshe,alishiriki katika kukuza Mikakati ya Kitaifa ya kuzuia VVU / UKIMWI nchini Kenya na nchi zingine ikijumuisha Afrika Kusini, Swaziland, Rwanda, Benin, Somali, Kongo  Brazzaville.

Alishiriki kikamilifu kuwapa ushauri wahanga wa milipuko kama vile Bomu jijini Nairobi ,uliotokea Agosti 7, 1998, na mashambilishi ya kigaidi ya Westgate ya mwaka wa 2013.

Pia aliongoza Timu za Ushauri wa Matibabu kwa waadhiriwa wa ajari za ndege ya Kenya huko Abidjan Cote d'Ivoire mwaka wa  2000 na ile ya Duala Cameroon mwaka wa  2007.

Alipokuwa  Mkurugenzi mratibu wa mipango  ya VVU na UKIMWI,alifanya juhudi  ili kupunguza maambukizi kutoka asilimia 14 hadi asilimia 5.6 hivi sasa.


Jumatano, 24 Julai 2019

Dolutegravir(DTG) dawa ya VVU


Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza dawa ya Dolutegravir(DTG) katika mapambano yake dhidi ya virusi vya Ukimwi,licha ya dawa hiyo kushukiwa kuwa na madhara kwa akina mama waja wazito.

Pendekezo hili limetolewa siku mmoja baadaya ya shirika hilo ,kuchapisha taarifa inayoonyesha  kuwa mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi bado yanaendelea.

Image result for dolutegravir
WHO inapendekeza  matumizi ya Dolutegravir(DTG) kama njia ya kwanza na ya pili ya matibabu  kwa watu wote,wakiwemo akina mama wajawazito na pia wenye uwezo wakupata ujauzito.

Tafiti za awali, zilitia shaka  uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya dawa ya DTG na tatizo linalosababisha watoto kuzaliwa na tundu kwenye uti wa mgongo na ubongo,yaani Spinal bifida.

Tatizo hili hutokea punde tu mama anapopata ujauzito huku akitumia dawa ya DTG.

Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zilitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya dawa ya DTG baadaya ya utafiti uliofanywa nchini Botswana kuonyesha kuwa dawa hiyo ilikuwa na madhara kwa wanawake wajawazito,mwaka uliopita.
Utafiti ulibaini visa vinne vya matatizo hayo kati ya wanawake 426 ambao walipata ujauzito wakati wakitumia dawa hizo za DTG.
Kufuatia utafiti huo,Kenya na  nchi nyingi ziliwashauri wanawake wajawazito na wanawake wanao tarajia kubeba ujauzito, kumeza dawa za efavirenz (EFV) badala ya DTG.
Hata hivyo ,baada ya  majaribio ya kisayansi ya kuchunguza ufanisi na usalama kati ya DTG na EFV barani Afrika, sasa ni dhahiri kuwa  kiwango cha hatari ya kupata tatizo la uti wa mgongo na  ubongo ni ndogo mno kinyume na  ilivyokuwa imekadiriwa hapo awali.
Shirika la Afya Duniani ,inasema kuwa DTG ni dawa ambazo zina ufanisi zaidi, rahisi kumeza na zina madhara machache kuliko dawa zingine ambazo zinatumika kwa sasa.
Katika harakati za kupambana na VVU, nchi zinazo endelea 82 ziliripoti kurudia matibabu ya VVU yanayotumia DTG.
WHO inatia mkazo mapendekezo mapya  yaliyoboreshwa na yanayolenga kusaidia nchi zaidi kuboresha sera za afya.
Kufuatia hayo,WHO imeandaa kikundi cha ushauri wa wanawake wanaoishi na VVU kutoka katika Nyanja mbalimbali ili kutoa ushauri katika masuala ya sera zinazohusiana na afya zao, na  zile za afya ya uzazi. 
DTG ilipendekezwa mnamo Juni 2017 kama dawa mbadala ya wanaougua Ukimwi na ambao hawakupata matokeo mema kwa kutumia dawa ya Efavirenz au zile za ARV.
Kenya ilikuwa nchi ya kwanza  barani Afrika kutumia dawa ya Dolutegravir(DTG).

Jumatano, 17 Julai 2019

chanjo ya polio(polio vaccine)


Maisha ya watoto milioni ishirini yako hatarini kufuatia taarifa za umoja wa mataifa kuwa watoto hawakupata chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilika mwaka wa 2018.

Magonjwa yanayozuilika ni kama vile,ugonjwa wa kupooza surua,Dondakoo na pepo punda.

Takwimu hizi zimetolewa na  shirika la afya dudniani(WHO) kwa ushirikiano na Shirika la watoto duniani (UNICEF).

Huku chanjo asilimia 86% ikitolewa kuokoa maisha ya watoto,bado kiwango kinachotakiwa cha asilimia 95% duniani kote hakijafikiwa.

Tangazo hili la umoja wamataifa linatia hofu huku ikifahamika kuwa mlipuko Zaidi waweza kutokea endapo hali hii haita shughulikiwa ipasavyo.

Shabaha ya kutoa chanjo ni kuimarisha afya ya watoto na kuepusha hatari ya milipuko ya wagonjwa yanayozuilika.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kuwa huduma ya chanjo ni muhimu ili kuzuia milipuko ya magonjwa.

Kiwango cha chanjo kwa watoto wasiopata chanjo hasa ni kutokana na hali ya ukimbizi inayosababishwa na vita nchini mwao.

Nchi hizi ni Afghanistan,Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,Chad, Congo DRC, Ethiopia, Haiti, Mali, Iraq, Niger, Nigeria, Pakistan, Somalia, Sudan Kusini, Syria na Yemen.

Matokeo haya yanaabatana na hali ilivyo nchini Kenya kuhusiana na chanjo ya ugonjwa wa kupooza na chanjo zingine.Inadaiwa kuna kuna upungufu au ukosefu wa chanjo  hospitalini hasa za umma.

Kumekuwa na tuhuma kuwa wazazi wanalazimika kulipa shilingi elfu nane hadi kumi na mbili katika hospitali za kibinafsi ili watoto wao wapate chanjo wanapozaliwa.

Mtoto anapozaliwa anahija kupewa chajo ya kupooza.Chanjo hii hupewa mtoto kupitia kwa mdomo, dozi tatu, halafu baadaye anadungwa shindano anapotimiza miaka mitatu na nusu.

Kinaya ni kuwa Kenya imekuwa katika mstari wa mbele kufanya kampeni dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza (Polio) katika maeneo tofauti nchini.

Zaidi ya hayo,kampeni nyingine ya Polio inatarajiwa kufanyika katika sehemu kadha,huku watoto 2.6 millioni walio chini ya miaka mitano wakitarajiwa kupata chanjo.

Majimbo yaliolengwa katika kampeini ya chanjo ya Polio ni  Mombasa,Tana River,Lamu,Kilifi,Isiolo,Turkana ,Nairobi,Wajir,Garissa na Mandela.

Mwaka 2018 idadi ya watoto walioshambuliwa kwa ugonjwa wa Surua ilikuwa ni 350,000
Kiwango hiki ni mara mbili ya idadi ya watoto walioshambuliwa katika kipindi cha kwa mwaka 2017.

Henrietta Fore Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, anasema, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujizatiti vilivyo kutoa chanjo ya kinga kwa kila mtoto duniani.





Ebola Goma



Ebola Goma

Shirika la Afya Duniani(WHO) litafanya kikao cha dharula hii leo kutathmini hatari ya Ebola nchini Congo.

Mkutano huu unafanyika siku moja, baada ya kifo cha kasisi mmoja aliyefariki baada ya kusafiri Butembo kufanya maombi.

Taarifa inasema mhubiri huyu alizuru eneo la Butembo ambalo ni baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na ugonjwa wa Ebola kwa muda.

Katika shughuli zake za maombi aliguza wagonjwa na huenda hapo ndipo alipoabukizwa maradhi hayo makali.

Alirudi Goma huku anaumwa na punde alipoenda kutafuta matibabu kwenye zahanati ,akapatikana na ugonjwa wa Ebola.

Moja kwa moja wataalamu wa afya wakachukua hatua kumsafirisha moja kwa moja hadi Butembo kupokea matibabu ya dharula, lakini kwa bahati mbaya akafariki.

Goma ni mji ulio na idadi ya watu milioni moja ,kwenye pwani ya Ziwa Kivu, karibu na Rwanda. 

Ni mara ya kwanza ugonjwa huu kuripotiwa Goma huku wasiwasi ukitanda katika nchi jirani ya Rwanda.Kuna shughuli nyingi hufanyika kila siku mpakani ,hasa katika mji wa Gishenyi.

Serikali ya Rwanda imesema itakuwa hatua ya dharula mpakani kwa kutoa tahadhari kwa  wananchi wake ili kuepuka kupata ugonjwa wa Ebola.

Mkutano wa leo unatarajiwa kutoa hatua au mikakati itakayofuatwa kuukabili ugonjwa wa Ebola ambao ni tishio nchini Congo na pia nchi Jirani.

WHO inafanya kikao baada ya Mkurugenzi Mkuu , Dkt Ghebreyasus kuzuru Congo kufuatia mripuko wa Ebola katika maeneo ya Butembo na Katwa.

Kwenye taarifa,Dkt Ghebreyesus alitoa hakikisho kuwa Shirika lake litajitahidi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola umekabiliwa.

Takribani wahudhumu wa afya elfu tatu,3000 wamepata chanjo ya Ebola huko Goma.

Zaidi ya watu 1650 wamefariki kutokana na maabuziki ya mapya,huku waabukizi 12 yakiripotiwa kila siku.