Trachoma (Vikope)
Trachoma au vikope
ni ugonjwa unaosababisha upofu.isitoshe,maabukizi yake yanatokana na bakteria
aina ya Klamidia Trakomati.
Ugonjwa huu unaweza kuthibitiwa ukitibiwa mapema.
Mazingira machafu na
ukosefu wa maji safi huchangia maabukizi ya maradhi haya.
Nchini kenya jamii
za wafungaji wa kuhamahama huadhrikika Zaidi.
Tafiti zinaonyesha
kuwa ,kati ya nchi 44 ambazo ziko Afrika na Asia, zilikubwa na ugonjwa
huu lakini umethibitiwa kwa kiwango cha juu kwa sasa.
Mbali na
hayo,serikali ya Kenya imeweka mikakati ya kutokomeza tishio hili .
Mwaka wa 2015,Wizara
ya Afya ilizidua mpango na miradi ili kuhakikisha Trachoma imekabiriwa mwaka
2019.
Mpango huu wa miaka
mitano, ambao unatarajiwa kukamilika mwaka huu ulilenga kufanya upasuaji wa
macho 40,000-katika maeneo yaliyo adhirika Zaidi.
Kajiado,Samburu,isiolo,Laikipia,Baringo,Turkana,Meru
Kaskazini ni baadhi ya maeneo 12 yaliotarajiwa kufaidika na mpango wa kukomesha
Trachoma.
Watu Zaidi ya 2.9
millioni watapata matibabu, elimu ya afya ya umma kuhusu Trachoma,jinsi ya
kujikinga, namna yakudumisha usafi na mazingira masafi.
Hii ni hatua nzuri kwa
serikali kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya ya Trachoma kwa
kuendelea kutoa dawa katika wilaya 12 zilizotajwa na kuwafanyia upasuaji
wagonjwa ambao wamefikia hatua ya kupata upofu.
Serikali ya Kenya imekua ikishirikiana na serikali
Uingereza kupitia taasisi ya UK aid na Queen Elizabeth Diamond Jubilee
Trust na shirika la Ugeremani la Christian Blind Mission katika kuhakikisha
wagonjwa wa Vikope wanafikiwa na kupata huduma za matibabu pamoja na kufanyiwa
upasuaji kwa wale ambao walio kwenye hatari ya kupata upofu.
Majimbo ya Kajiado na Samburu yanaongoza kwa
kiwango cha juu cha Trachoma.
Dalili
·
Macho
kuwa mekundu.
·
Macho
kutoa machozi kila wakati.
·
Maumivu
na kuwasha macho.
Madhara
·
Kushindwa
kustahimili mwanga na maumivu ya macho kwa watoto.
·
maamivu
makali mgojwa anapopepesa macho kutokana na kuchomwa na vikope
·
kufifia
uwezo wa kuona.
·
upofu
kutokana na makovu kwenye kioo cha mbele ya jicho.
· Kinga
·
Kudumisha
usafi wa mwili na mazingira ya makazi .
Matibabu
·
Matibabu
ya mapema hupunguza vimelea vinavyoleta ugonjwa huu
·
Operesheni
ndogo, kwa wagonjwa waliokwisha kupata vikope.