Uterine Fibroid Embolization
Je wajua kuwa ugonjwa wa fibroids yaani uvimbe au vivimbe ambavyo huwa kwenye ukuta wa kizazi (uterus) waweza kutibiwa na mwanamke akawa hana matatizo tena kwenye uzazi wake?
Kwa mujibu wa daktari, Timona Obura, ambaye ni mtaalam (Gynaecologist) katika hospitali ya Aga Khan, Hii inawezekana kutokana na tecnhologia ya kisayansi ambayo inajulikana kama Uterine Fibroid Embolization.
Vivimbe hivyo vinaweza kuwa vidogo Kama ncha ya kidole au vikubwa Kama viasi .Pia vinaweza kugunduliwa, kwa kutumia tecnologia inayojulikana kama Ultrasound.
Mwanamke anaweza akawa kwenye hatari ya mimba kutoa(miscarry) kwani,uvimbe unaweza kujaa kwenye sehemu anayokaa mtoto.
Ingawa kuna aina za upashuaji zinazotumiwa kuondoa Fibroids,Daktari Obura anasisitiza kuwa Embolization ni namna maalum ambayo haihitaji upasuaji wa kawaida.Pia hamna madhara kama upasuaji wa kawaida.
Hapa mwanamke au mgonjwa anaelimishwa kuhusu jinsi upasuaji unavyofanywa,faida na jambo lolote analostahili kufahamu kabla hajafanyiwa upasuaji.
Hii binu ni muhimu kwa wale wanaotarajia kupata watoto siku za badaye.Pia kuna afueni kwani fibroids hazirudi tena.
Hata hivyo kuna upasuaji kama vile (Hysterectomy) hapa mwanamke anatolewa kizazi chote na hawezi kutunga mimba tena.Hii hufanywa kwa mwanamke ambaye Fibroid ni kubwa ,nyingi na pia hana haja au lengo la kuzaa tena.
Myomectomy ni namna pia ya upasuaji, ambapo mwanamke hutolewa Fibroids tu na kuacha kizazi.Ikiwa Fibroid ni moja au chache na si kubwa sana, mwanamke anaweza kuendelea kuzaa.Hii ni shuluhu ya muda tu kwa maana fibroids zinaweza zikarudi.
Kuzuia ni bora kuliko kuponya,wale wanaugua ugonjwa huu wanaweza kuamua wenyewe au kwa usaidizi wa Gynaecologia wake.
Kuzuia ni bora kuliko kuponya,wale wanaugua ugonjwa huu wanaweza kuamua wenyewe au kwa usaidizi wa Gynaecologia wake.
Pia ni muhimu kutafuta matibabu ya haraka unapougua,kuepukana na hatari.
-Dalili za ugonjwa wa Fibroids ni kama vile kuvuja damu kwa wingi wakati wa hedhi na Kuumwa na tumbo.
Kwa mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa fibroid tutakuwa kunaalika maoni kutoka kwa mashabiki wanaotembelea mtandao huu.
Yote mwakaribishwa kutoa maoni au kuuliza swali.
Huyu daktari hadi sasa yupo hapo Agha Khan nina ndugu yangu uvimbe na tunahitaji msaada wake.... Napatikana kwa 0784587191
JibuFutaYupo
JibuFutaDr Timona Obura
Agah Khan University Hosp
+254 203662876
okey thanx
JibuFuta