Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2020

Silas Njiru-Askofu

Picha
Askofu mstaafu Silas Njiru Afariki dunia Virusi vya Corona vimepokonya kanisa katoliki na Kenya kwa jumla Askofu Mstaafu wa Jimbo la Meru,Silas Njiru . Askofu Njiru alifariki mapema Jumanne nchini Italia baada ya kuambukizwa Covid-19. Askofu wa Meru Salesius Mugambi ambaye alichukua hatamu za uongozi wa jimbo hilo baada ya kustaafu kwa marehemu, alisema Askofu huyo mstaafu alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Rivoli ambapo alikuwa amelazwa kwa siku tatu. Hapo awali Asofu wa jimbo la Embu kupitia ujumbe kwenye mtando, aliomba wakristo kumuombea Marehemu kwani alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi .   Alikuwa miongoni mwa mapadre   watatu walioambukizwa virusi vya Corona kwenye makao yao. Marehemu alikuwa akikaa katika nyumba ya Mtakatifu Joseph Allamano huko Alpignano, Turin, Italia tangu kustaafu kwake. Alizaliwa Mwezi 1928 katika kijiji cha Kevote, Kaunti ya Embu. Alihudhumu katika jimbo la Meru kwa muda mrefu zaidi,pia amekuwa Padre kwa miaka...

COVID 19 Kenya

idadi ya maambukizi yaongezeka kenya Idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa COVID 19 imefikia 374 baada ya watu wengi 11 kupatikana na maambukizi. Kati ya visa 11 mpya, saba ni kutoka Jimbo la Nairobi na nne kutoka Mombasa. Walioambukizwa wakiwa kati umri wa   miaka mitatu na 70. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za   Wizara ya Afya ya Kenya .   Kaimu Katibu Mkuu wa Afya Rashid Aman,amesema   idadi ya watu wote waliopona sasa wamefika 124 baada ya watu wengine 10 kuopona baada ya masaa ishirini na nne. Kuna visa vipya katika maeneo manne Nairobi,   manne yalikuwa kutoka Kawangware, na mengine kutoka maeneo ya Eastleigh, Manji na Kaloleni. Dkt Aman ametowa wito kwa maafisa wa polisi kuhakikisha harakati na mbinu   za kuigia ndani na nje ya kaunti hizi mbili zinazingatiwa   kuzuia kuenea kwa virusi hivyo ambavyo vimewaambukiza zaidi ya watu milioni 3 na kuwauwa watu 212,337 ulimwenguni. Wizara ilifafanua zaidi kwamba baa zitab...

Malaria 2020

Siku ya malaria yaadhimishwa huku maambukizi  ya janga la Corona yakiendelea kuongezeka.
COVID 19 Maambukizi yaongezeka Tanzania Idadi ya wagonjwa wa COVID 19 imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini Tanzania. Hii leo visa 30(thelathini) vimeripotiwa huku idadi ya maambukizi ikifika 284. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa litoa taarifa ya maambukizi zaidi   wakati wa maombi ya taifa   jijini Dar es Salaam leo.  Majaliwa alisema kufikia jana   wagonjwa 256 wanaendelea vizuri huku saba wakiwa kwenye uangalizi maalumu. Idadi ya waliofariki ni 10 huku 11 wakipona. Waziri Mkuu ,Bw. Majaliwa amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona vimedhibitiwa . Amesema serikali inatoa eimu kwa umma jinsi ya kujikinga,kamati ya kitaifa imeundwa ili kufuatilia hali ya ugonjwa nchini na pia timu ya wataalamu wa afya imeundwa ili kushughulikia swala hili. Bw.majaliwa amewataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya wataalamu wa afya na serikali ili kuepuka athari Zaidi ...
COVID 19 Maambukizi yaongezeka Tanzania Idadi ya wagonjwa wa COVID 19 imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini Tanzania. Hii leo visa 30(thelathini) vimeripotiwa huku idadi ya maambukizi ikifika 284. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa litoa taarifa ya maambukizi zaidi   wakati wa maombi ya taifa   jijini Dar es Salaam leo.  Majaliwa alisema kufikia jana   wagonjwa 256 wanaendelea vizuri huku saba wakiwa kwenye uangalizi maalumu. Idadi ya waliofariki ni 10 huku 11 wakipona. Waziri Mkuu ,Bw. Majaliwa amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya virusi vya Corona vimedhibitiwa . Amesema serikali inatoa eimu kwa umma jinsi ya kujikinga,kamati ya kitaifa imeundwa ili kufuatilia hali ya ugonjwa nchini na pia timu ya wataalamu wa afya imeundwa ili kushughulikia swala hili. Bw.majaliwa amewataka watanzania kuchukua tahadhari kwa kufuata maagizo ya wataalamu wa afya na serikali ili kuepuka athari Zaidi ...

Virusi vya COVID 19

chimbuko la Virusi vya Corona  Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kuwa hakuna ushahidi kuwa  wa virusi vya Corona vilitengenezewa kwenye maabara. Hata hivyo Msemaji  wa shirika hilo, Fadela Chaib amesema  ushahidi  uliopo unadhihirisha  kuwa virusi vya corona vilitoka kwenye wanyama nchini China mwishoni mwa 2019.  Akihutubia  mkutano wa waandishi habari mjini Geneva, alisema kuna uwezekano mkubwa vilitoka kwenye popo.Zaidi ya hayo,anasema haijabainika ni vipi virusi hivyo vilitoka kwenye popo na kuingia kwa binaadamu.  Hapo awali, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa serikali yake inajaribu kubaini kama virusi hivyo vilitengenezwa kwenye maabara katika mji wa Wuhan nchini China, ambako janga la virusi vya corona lilianzia Desemba mwaka uliopita. Kumekuwa na maoni na misimamo tofauti kuhusu ni jinsi gani virusi vya Corona vilikotoka huku wengi wakijadili kuwa vilitoka kwa wanyama huku wengine wakisema vilisababishwa au...

Corona Virusi jikinge

Upuka maambukizi ya Corona;fuata masharti au maagizo Tangu mlipuko wa virusi vya Corona kutangangwa kimekuwa na mijadala na maoni tofauti dhidi ya kijikinga na virusi. Wataalamu wa afya wako kwenye harakati za kutafuta kinga ya maradhi haya huku Shirika la Afya Duniani likionya dhidi ya Imani potuvu kuhusu tiba ya corona inayotolewa na baadhi ya   watu. Baadhi ya dhana za kupotosha kuhusu tiba ya COVID -19 ·          Kunywa vileo ·          Kunywa chai ya rangi ·          Kuoga maji moto ·          Kukaa kwenye jua ·          Ulaji wa vitunguu saumi na timu ·          Mbu inaambukiza virusi vya Corona  Hizi ni dhana potofu ambazo hazina ukweli wowote. Hivyo basi, ni muhumu kuhakikisha : ·  ...

Askofu Getrude Rwakatare

Picha
MAMA GETRUDE RWAKATARE AFARIKI DUNIA Kifo cha Askofu Rwakatare kimepokelewa na waliomfahamu kwa huzuni na majonzi. Mawanawe Muta Rwakatare,alitoa taarifa ya kifo cha mamake.Anasema Askofu alikuwa na matatizo ya moyo na alifariki hospitalini ambapo alipelekwa baada ya kuugua ghafla.   Alikuwa ni mtumishi wa Mungu,Mbunge maalum na mwanabiashara mashuhuri nchini Tanzania Askofu Daktari mama Rwakata alikuwa na maneno na sauti   nyororo ya kumtoa nyoka pangoni. Mahubiri yake yalikuwa na warsia na alinena kwa ukakamavu wa mama shujaa. Nakumbuka wakati mmoja nilipozuru Dar es salam ,marafiki wangu wakanikaribisha kutembelea kanisa la Mlima wa moto pale mikocheni B. Nilipoketi na kusikiriza mafunzo/mahubiri yake mama Rwakatare nilijihisi kama nimezaliwa tena kiroho, tangu wakati huo nilipenda kusikiliza mahubiri yake   kwenye televisioni . Alikuwa kwenye mstari wa mbele kwenye maswala ya usawa wa jinsia hasa maswala na kina mama na maendeleo. Wak...

COVID 19

Picha
Shirika la Afya Duniani, (WHO) limetangaza ongezeka ya maambukizi na vifo vya virusi vya Corona. Takwimu zinaonyesha ongezeko ya maambukizi hadi milioni 2 kufikia sasa,huku vifo vikiwa elfu 131. Marekani na mataifa ya Uropa yanaongoza katika vifo na maambukizi duniani. Marekani  vifo elfu 28,326 na maambukizi elfu 637. Ikifuatiwa na Italiano na vifo 21,645,Uhispania nayo ni ya tatu na maafa ya kiwango cha 18,579. Ufaransa inachukua nafasi ya nne   na vifo Zaidi ya elfu 17 huku Uingereza ikiwa ya tano na vifo elfu 12. Tarifaa hii inatolewa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha mswada wa fedha kwa Shirika la Afya Duniani kwa kile alichokitaja kama kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maambukizi ya Corona na pia kuelekeza juhudi zake nyingi Uchina katika shughuli za kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Hata hivyo, hatua ya Trump imeshutumiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kwani haukuwa wakati mwafaka wa kuchukua h...

Ken Walibora amefariki

Picha
Ken Walibora ameaga dunia. Mwandishi wa Riwaya ya Siku Njema na wanahabari mtajika Ken walibora amefariki . Inadaiwa mwanahabari/mtangazaji alipatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali kuu ya Kenyatta. Marehemu aligongwa na gari katika barabara ya Ladhies na gari la usafiri wa umma siku ya Ijumaa. Hakika Walibora alitukuza kiswahili.... Walibora amechangia katika maendeleo ya Lugha hasa ya Kiswahili kwa kuandika vitabu kama vile Siku Njema na Kidagaa kimemwozea,Ndoto Ya Amerika ,nasikia sauti ya mama,Ndoto ya Almasi ,Kufa Kusikana  na vingine vya kimombo. Zaidi ya hayo,Walibora alifanya kazi na kampuni ya Utangazaji ya Nation kama mhariri wa kitengo cha kiswahili. Baadaye alisafiri hadi Marekani alipokuwa mhadhiri wa lugha ya afrika. Kifo chake kimetokea baadaya waandishi wawili wa kampuni ya Nation kugongwa na gari katikati mwa jiji la Nairobi. Mola amlaze pema peponi ustadh,malenga Walibora

Donald Trump asitisha WHO msaada

Picha
Shirika la Afya Duniani, (WHO) limetangaza ongezeka ya maambukizi na vifo vya virusi vya Corona. Takwimu zinaonyesha ongezeko ya maambukizi hadi milioni 2 kufikia sasa,huku vifo vikiwa elfu 131. Marekani na mataifa ya Uropa yanaongoza katika vifo na maambukizi duniani. Marekani imerekodi vifo elfu 28,326 na maambukizi elfu 637. Ikifuatiwa na Italiano na vifo 21,645,Uhispania nayo ni ya tatu na maafa ya kiwango cha 18,579. Ufaransa inachukua nafasi ya nne   na vifo Zaidi ya elfu 17 huku Uingereza ikiwa ya tano na vifo elfu 12. Tarifaa hii inatolewa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha mswada wa fedha kwa Shirika la Afya Duniani kwa kile alichokitaja kama kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maambukizi ya Corona na pia kuelekeza juhudi zake nyingi Uchina katika shughuli za kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Hata hivyo, hatua ya Trump imeshutumiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kwani haukuwa wakati mwafaka wa kuchukua hatu...