Aliyekuwa Rais was Burundi Pierre Buyoya afariki ncini Ufaransa.
Kulingana n'a binamuye, kiongozi huyo aliyetawala Burundi kwa kiimla alifiki baada ya kuugua maradhi ya COVID-19..
Aliyekuwa Rais was Burundi Pierre Buyoya afariki ncini Ufaransa.
Kulingana n'a binamuye, kiongozi huyo aliyetawala Burundi kwa kiimla alifiki baada ya kuugua maradhi ya COVID-19..
CHANJO DHIDI YA COVID -19
Tangu virusi vya Corona kutangazwa
kama janga la ulimwengu,sekta nyingi zimeadhirika hususan ile ya elimu.
Watoto wanaostahili kuwa shuleni
wamelazimika kusalia nyumbani huku serikali ikitafuka mbinu za kuhakikisha
masomo yemerejelewa bila kuhatarisha Maisha ya Watoto.
Nchini Kenya hatua mwafaka tayari
zimeafikiwa kuhakikisha kuwa baadhi ya wanafunzi wamerejea shuleni huku
wakihakikisha masharti ya kukabiliana na Virusi ya Corona inapewa kipao
mbele.
Isistoshe,kuna haja ya
kuwachanja Watoto Pamoja na waalimu punde tu chanjo zitakapofika kwenye nchi
mbalimbali duniani.
Kulingana na taarifa za shirika
la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF chanjo
dhidi ya COVID- 19 itakuwa hatua muhimu ya kurejesha hali ya masomo katika
mstari wa kwanza.
Bi. Henrietta Fore, Mkurugenzi
Mtendaji wa UNICEF anasema huku ugonjwa wa COVID-19 ukifika kilele na
kupelekea shule kufungwa ,sekta ya elimu uliadhirika pakubwa huku asilimia 90
ya Watoto kote duniani wakibaki nyuma kimasomo.
Hata hivyo anashauri kuwa serikali
zichukua hatua kutoa chanjo kwa Watoto na wanaowatunza hasa walimu,baada
ya wahudumu wa afya walio msitari wa mbele na makundi mengine yaliyo
hatarini zaidi ya kuambukizwa COVID-19.
Ingawa kuna wale wanaohofia kurejea masomo
kutahatarisha Maisha ya Watoto, Bi. Fore anasema kutofanya hivyo
kutachangia Watoto wengi kukataa au kutoendelea na masomo katika umri mdogo na
pia kwa wazazi wao kutoendelea na shughuli za kutafuta riziki -za kila siku.
Ingawa maamuzi ya kutoa chanjo hizo yako
mikononi mwa serikali, “athari za kuendelea kukosa au kutohudhuria masomo
ni kubwa sana hususan kwa watu wasiojiweza,amesema Bi. Fore.
Haya yanajili huku
nchi ya Kenya ikitarajia kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Korona kuanzia
mwezi wa Januari mwaka wa 2021.
Chanjo hiyo ya Oxford University-AstraZeneca itawalenga Wahudumu wa afya, maafisa wa polisi, wakongwe na walimu.
Wengine watakao pata
chanja kwa awamu ya kwanza ni wale ambao kazi zao zinawasabisha kuwa miongni
mwa umati na wenye maradhi sugu ,imesema Wizara ya afya .
Waziri wa Afya Mutahi
Kagwe, amesema kwamba Kenya itapokea chanjo milioni 24 kabla ya kushirikiana na
kamapuni za taifa la Uchina.
Kagwe amesema kwamba
Astrazeneca ni za bei nafuu ikilinganishwa na Pfizer ambayo
inastahili kuhifadhiwa katika mazingira ya -70° c.
Serikali inasema kuwa
Wakenya watapokea dozi hizo milioni 24 bila malipo kwani zimefadhiliwa na
Shirka la Kitaifa la Chanjo GAVI.
Gavana Wa Jimbo La Nyamira Aaga Dunia
Gavana wa Kauti ya Nyamira John Obiero Nyagarama afariki dunia.Nyagarama
amekuwa akipokea matibabu katika Nairobi hospital iliyoko jijini Nairobi,kwa
takriban mwezi mmoja.
Inasemekana Gavana
Nyagarama alikuwa anaugua ugonjwa wa COVID-19.
Kulinagana na familia
yake,alikuwa na matatizo ya kupumua baada ya mapafu yake kushindwa kufanya
kazi.
Hata hivyo, Nyangarama
amekuwa na matatizo ya kiafya ila familia yake imesita kusema alichokuwa anaungua
.
Zaidi ya hayo,
alisifika kwa kufanya miradi ya maendeleo kwenye kauti ya Nyamira, na pia
kuwahimiza wakaazi umuhimu wa kujizuia kuambukizwa virusi vya Corona.
Pia
, alikuwa
mkulima Hodari has awa zao la chai.Alifanya kazi katika sekta ya kilimo hususan
majani chai na kupanda ngazi kwa kasi hasi akawa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chai nchini kwa
muda mrefu.
Hapo awali alifunza
katika shule mbalimabli baada ya kufuzu kama mwalimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi.Hadi
kifo chake alikuwa na umri wa miaka 74.
Mola ailaze roho
yake mahali pema peponi.