Uzazi wa mpango Ni ile hali ya mume na mkewe kukumbaliana jinzi au namna ya kupunguza mimba zisizotarajiwa. Serikali ya kenya imetilia mkazo umuhimu uzazi wa mpango.Zaidi ya hayo, kuna namna na aina tofauti za uzazi wa mpango. Kuna vidonge vya kumeza, shindano ijulikanayo kama Depo provera, Vijiti, kitanzi, mpira wa mama au baba,kufunga kizazi kwa mama au baba na njia za asili. Ukweli ni kuwa, ni mpira pekee kati ya aina zote za mpango wa uzazi inayozuia maambukizi ya ugonjwa. Aina zinginezo hazizui kupata magonjwa ya zinaa na pia virusi vya ukimwi. Bali na hayo, kuna dhana potofu kwa baadhi ya watu wanaoamini kuwa matumishi ya auna hizi zote za uzazi wa mpango zinazuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa na virusi ya ukimwi. Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika moja la afya la Marekani na kuchapishwa na jarida la The Lancet, akina mama wanaotumia aina hii ya upangaji uzazi wako hatarini ya kuambukizwa au kuwaambukiza waume wao virusi vya HIV,kuliko w...