Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2012

WHO Malaria Kenya

Picha
Kenya yatoa ripoti zisizo kamili Serikali ya Kenya imepiga hatua kukabiliana na ugonjwa wa malaria,ingawa hatua zake hazijaridhisha Shirika la Afya Duniani. Kulingana na ripoti iliyotolewa rasmi na Shirika la Afya Duniani(WHO),tathmini ya maendeleo ya Kenya kupambana na malaria haiwezi kufanywa kwa sababu takwimu zake si kamili kudhibitisha juhudi zake za kuukabili ugonjwa wa malaria. WHO imetaja Kenya kuwa miongoni mwa nchi saba katika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambazo viwango vya maambukizi vingali juu,huku huduma za afya zikiwa mbali na wananchi. Zaidi ya hayo, serikali ya Kenya ilitoa ripoti kudhibitisha kutumia Dollar za Marekani 2,700,000 katika mipango yake ya kupambana na malaria katika mwaka 2010.Hata hivyo hakuna takwimu zinapatikana ama zilizotolewa katika kipindi za  2011. Katika kipindi za 2010 Kenya ilipata Dollar za Marekani 39,100,000 kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa iliyofadhiliwa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi , K...

Mandela hospitali

Picha
  Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea kupokea matibabu hospitali mjini Pretoria ambako anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu. Mzee Mandela alipelekwa na kulazwa hospitali, Jumamosi(wiki moja iliyopita). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea, Mandela naendelea kupata nafuu. Mapema mwaka huu, Mandela alilazwa hospitali ili kutibiwa matatizo ya tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu. Homa ya mapafu, husababishwa na viini tete vijulikanavyo kama (Streptococcus pneumoniae) na huathiri sehemu za kupumua kwenye mapafu . Bwana Mandela amewahi kutibiwa kwa mara nyingine ugojwa wa kifua kikuu unaoathiri mapafu. Magonjwa mengi ya mapafu hutibiwa kwa madawa , mgonjwa kupu mzika au kupata vinywaji vingi.     Wazee na watu ambaom hawakinga ya mwili ndiyo huadhiriwa na maradhi haya. Bwana Mandela ana miaka 94.

mkataba wa Kyoto

Picha
  Hatimaye mkutano wa kujadili mabadiliko ya hali ya hewa mjini Doha umeafiki kurefushwa Mkataba wa Kyoto hata baada ya   nchi ya   Urusi kujaribu kuyapinga mafikiano hayo. Wajumbe katika mkutano huyo, walijikaza kisabuni ili kupata suluhu katika hoja ambayo hakika ilikuwa ya dharula. Maji taka Mkutano huu uliwaleta pamoja wajumbe zaidi ya 17,000 kutoka nchi 200 duniani, uliafiki   kurefushwa Mkataba wa Kyoto unaodhibiti uzalishaji gesi za nyumba ya kioo hadi mwaka 2020.   Isitoshe,nchi 27 za Umoja wa Ulaya, Australia na Uswisi na nchi nyingine nane zenye maendeleo ya viwanda zimekubali kushikamana na makubalino ya kuzuia uzalishaji wa gesi hizo hadi mwaka 2020. Hata hivyo,Marekani imekataa kutia saini Mkataba wa Kyoto. Pia   makubaliano hayo hayazihusishi nchi zinazochafua kwa kiasi kikubwa mazingira kama China na India. Katika hotuba yake , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon,aliunga mkono hatua hiyo na kuzisitiza kuwa n...

pamoja tuangamize saratani

Picha
Ni muhimu kudumisha usafi kinywani.Kusungua meno baada ya kula ilikuepikana na magonjwa kama vile  Saratani ya mdomo.saratani hii husambaa kinywani kwenye ulimi na koromeo.Ugonjwa huu huchukua muda mrefu kabla kutambuli.Wanaovuta sigara,kuvuta tumbako au kunywa pombe wamo hatarini mwa kupata saratani ya mdomo. Saratani ya mdomo ina inaweza kutibiwa unaweza kitibiwa ukiwahiwa mapema. Ishara ya saratani yam domo ni kama zifuatazo;   Uvimbe sehemu yoyote mdomoni, ambao hauponi kutokuwa na damu kwa urahisi. Kufa ganzi mdomoni. Kuhisi uchungu unapo tafuna, kumeza chakula ulimi unapotumika. Kubadilika kwa sauti. Kuumwa na sikio. Koo linalowasha bila kupona. pamoja tuangamize saratani

Martin Shikuku aaga dunia-Saratani

Picha
Ugonjwa wa saratani umetupokonya mwanasiasa mkongwe mzee Martin Shikuku. Mzee Shikuku aliaga dunia katika hospitali ya Texas ambayo ni kituo cha  kipekee cha matibabu cha ugonjwa wa saratani. Shikuku alikuwa akipata matibabu katika kituo hicho kwa miezi kadha. Shujaa Shikuku alikuwa tayari alijizika akiwa hai kwa kujichimbia kaburi na kukamilisha kushughuli zingine ambazo zinaambatana na maziko. Mbunge huyo wa zamani wa Butere alikuwa mstari wa mbele katika harakati ya kutaka mfumo wa vyama vingi na pia mtetezi wa haki za wanyonge. Alijipata matatani na Uongozi wa rais mstaafu Daniel Moi alipoungana na viongozi wengine kuaada mkutano wa hadhara katika uwanja wa kamukunji, kutetea mvumo wa vyama vingi. Alifungwa lakini hakukoma kumkosoa viongozi wafisadi na waliojipenda na kusahau kuwakilisha wananchi inavyostahili. Kwake hayati Shikuku,siasa ilikuwa ni witu wala si kujinufaisha.Miezi miwili iliyopita Waziri Mkuu Raila Odinga alimtembelea hopitalini...
Picha
Waziri wa afya ya umma Beth Mugo apona kansa.ugonjwa wa kanza ume kuwa tishio hapa nchini Kenya na pia mataifa mengi ya Afrika. hata hivyo kulingana na waziri beth Mugo ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa na kupoona endapo utagunduliwa mapema. Akizungumza jana baadha ya kuasiri kutoka Marekani ambako amekuewa akipokea matibabu ya kansa, waziri Mugo ametangaza kuwa kenya itafungua kituo cha Kansa nchini ilikuwatibu watu wanaougua ugonjwa huo. Bi mugo aligunduliwa kuugua kanza ya matiti na kwa bahati nzuri iligunduliwa kabla haijaenea na kwa sasa anasema ako salama salimini. Pia waziri mugo alionya wakenya kuhakikisha kuwa wanaishi kwenye mazingira safi, kwani uhalibifu wa mazingira hunachangia kuenea kwa ugonjwa hatari wa kansa. "Hewa safi, mazingira mema na lishe bora ni muhimu kwa kuepa maradhi ya kansa. Ni jukumu letu kama wakenya kudumisha usafi na pia upanzi wa miti ili kupata hewa safi.Hii itakuwa ni njia moja ya kuepuka maradhi hatari ya kans...

Tohara-Ujeremani

Picha
Utata kuhusu tohara ya wanaume imetatuliwa baada ya Kansela wa Ujerumani kuunga mkono jamii za Kiyaudi na za Kiislaamu zinazo taka kitendo cha kutahiriwa kiendelee katika jamii zao. Mseamji wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert alisema " kutailiwa kwa watoto wa kiume ni kitendo ambacho kinakwenda sambamba na imani ya dini hizo na hakuna adhabu itakayo tolewa. "Na ieleweke serikali inaruhusu haki ya kiimani na Wayahudi na Waislaam ni Wajeruamani hivyo wanahaki sawa na Wajerumani wangine." Kuungwa mkuno huko kwa kitendo cha kutailiwa kumekuja baaada ya daktari mmoja kutokutwa na hatia ya kusababisha maumivu kwa mtoto aliye mtairi, ambapo ilidaiwa mtoto huyo alikutwa na matatizo ya kiafya kutokana kutailiwa huko. Hata hivyo kitendo cha kutailiwa kimekuwa kinaleta mvutano katika jamii nchi Ujerumani huku wengine wakipinga na wengine wakiunga mkono. Tohara ya mwanaume ni ile hali ya ukataji wa ngozi ya mbele inayoficha kichwa cha uume. Kulingana na wataal...

kongamano la afya ya uzazi London

Picha
Katika juhudi zake za kuboresha sera za uzazi , jumuia ya kimataifa   imeada mkutano wa kujadili uzazi wa mpango nchini   Ungereza. Mkutano huu wa kimataifa utajadili Uzazi wa Mpango kwa nchi maskini zaidi duniani. Baadhi ya viongozi wa Afrika walioalikwa kwenye   mkutano huu ni pamoja na ; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete , Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Mwenyeji wa mkutano huu ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroun. Mkutano ,huu wa siku moja umedhaminiwa na Serikali ya Uingereza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na Taasisi ya Bill and Belinda Gates Foundation. Ni mara ya kwanza mkutano wa aina hii unafanyika nchini Uingereza ,na utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Queen Elizabeth. Inakisiwa   utaanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi b...

Arafat

Picha
Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat watoa majibu nusu.  marehemu Arafat wakati akiwa mwenye afya nzuri  marehemu Arafat baada ya kuugua     Uchunguzi wa kisayansi uliyofanywa kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi na rais wa Wapalestina umetoa majibu nusu tangu kuanza kwa uchunguzi huo. Rais Yasir Arafat ambaye alifariki dunia nchini Ufaransa ambapo alipelekwa kwa ajili yamatibabu baada ya kuugua wakati akiwa amefungiwa  kutoka katika mji wa Ramallah na serikali Izrael.   Dr Francois Bochud ambaye ni mtaalamu wa Radiophysique iliyopo nchini Switzerland alisema " naweza kusema tumekuta aina ya gesi inayo julikana kama polonium-210 ambayo inaweza kuwa chanzo ca kifo chake na tunaweza kupata jibu sahihi ikiwa baadhi ya viungo vya marehemu Yasir Arafat vitapatikana kwa  uchunguzi zaidi."   Uchunguzi wa kifo cha Yasir Arafat ulikuja baada ya mkewe Suha Arafat  kuruhusu uchunguzi kuendelea na kutoa ruhusa ya kuwa mwili wa Yasir Araf ufu...

Kifua kikuu (TB)

Picha
Hatua za Kenya Kenya imepiga   hatua madhubuti   katika juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Kenya imeorodheswa 15 kwenye orodha ya nchi 22 ambazo ugonjwa wa kifua kikuu ungali ni tishio. Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani linaarifu kuwa juhudi za pamoja zimesaidia kupunguza vifo kwa asilimia 40 tangu mwaka 1990.   Watu milioni 46 wameponywa kuanzia mwaka 1995 kutokana na juhudi za Umoja wa Mataifa, serikali mbalimbali, wafadhili, makundi ya kijamii, washirika binafsi, wataalamu wa afya, na makumi ya maelfu ya watumishi wa idara za afya pamoja na familia na jumuiya zilizoathirika Umaskini na Virusi vya ukimwi unachangia pakubwa   katika maambukizi ya   kifua kikuu katika nchi zinazoendelea. Kwa kawaida, wagonjwa ambao wanapatikana na magonjwa ya kuambukiza mara kwa mara hutengwa kuzuia kueneza ugonjwa.Hii hufanyika katika wodi maalum katika hospitali za serikali. Mkurugenzi wa maradhi ya ki...

Mzee Nelson Mandela apata matibabu

Picha
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela aendelea kupata nafuu baada ya kutoka hospitalini , alikolazwa kutokana na maumivu ya tumbo ambaye yamekuwa yakimtatiza kwa muda mrefu. Hapo awali, taarifa kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma ilisema Mzee Nelson Mandela alilazwa hospitalini na akawaomba   Waafrika Kusini kumuombea nafuu ya haraka. Mzee Mandela, mwenye umri wa miaka 93 hajaonekana hadharani kwa muda mrefu sasa kufuatia kudorora kwa afya yake . Wananchi wengi nchini Afrika Kusini walipokea habari za kulazwa kwake hospitalini kwa hofu na huzuni tele, lakini wakasema wanaendelea kumuombea apate afueni ya haraka. Mbali na hayo,mzee Mandela aligunduliwa   kuugua saratani ya tezi dume,2001 na baada ya matibabu akapona, kwani iligunduliwa mapema. Alikuwa Rais wa kwanza mweusi katika nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 na kisha akaachia ngazi mwaka 1999. Mandela anatambulika kote duniani kwa juhudi zake za kupambana na utawala wa kibaguzi wa Makaburu kwa muda mrefu na...

Njenga Karume aaga dunia

Picha
Marehemu Njenga Karume  Aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa zamani wa Kiambaa, Njenga karume amefariki dunia. Karume ameaga dunia katika hospitali ya Karen hapa Nairobi ,alipokuwa akipokea matibabu, baada ya kuugua saratani. Marehemu Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 83. Rais Mwai Kibaki ametoa salamu zake za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Marehemu huku akisema amempoteza rafiki wa dhati. Karume alikuwa kigogo wa siasa na alimuunga mkono rais Mwai Kibaki katika juhudi zake za kuimarisha siasa za chama cha Democratic party(DP). Karume alikuwa mwanabiashara mashuhuri ambaye alikuwa na bidii kama za mchwa.Alijizatiti kuwa mmojawa   matajiri watajika hapa nchini,licha ya kuanzia chini sana. Katika kitabu chake, alichoandika kuhusu maisha yake, Karume alisema vile alijitahidi kutoka uchomaji wa makaa hadi dhahabu. Anatajwa pia kama aliyepigania uhuru, aliyehakikisha tamaduni zinahifadhiwa. Alikuwa mbunge wa kiamba lakini 2007 alipoteza kiti ...