Alhamisi, 1 Desemba 2016

Aids vaccine


Leo ni siku ya Ukimwi Duniani.
Maadhimisho haya yanakuja wakati  ufanisi kukabiliana na janga la Ukimwi ukichukua mwelekeo mwafaka.

Hii ni kufuatia tangazo kuwa Afrika Kusini inafanya majaribio chanjo mpya dhidi ya virusi vinavosababisha Ukimwi.
Endapo itapata mafanikio, chanjo Hii itawezesha waadhiriwa wa ugonjwa huu, kukabiliana na makali ya virusi (VVU).

Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.

Wanasayansi matumaini majaribio hayo, yanayojulikana kama  HVTN 702, yatazinduliwa  kwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanaojamiiana kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.Wagonjwa watakaoshiriki katika chanson hiyo wanapashwa kuwa n'a umri  wa kati ya miaka 18 na 35.

Hata hivyo kuna watu wanao sema kuwa chanson hii ina faida na hasara pia.
Itawasaidia wagonjwa wa Ukimwi huku wengine wakiamua kufanya ngono kihorera.

Pia Hii chanjo itakuwa na madhara kwa mwili kama vile;
Vipele , kizunguzungu na maumivu

Jumatatu, 28 Novemba 2016

TB


Tanzania imepiga hatua mbele, kwa kubuni mbinu ya kuukabili ugonjwa wa kifua kikuu, kwa kuzindua MAABARA  jijini Dar es salaam. Mradi huu utakua chini ya usimamizi wa chuo kikuu cha  Kilimo cha Sokoine.

Ubunifu huu utafanywa kwa kutumia panya buku kupima sampuli za ugonjwa wa kifua kikuu (TB).Inaaminika panya mmoja ana uwezo wa kupima sampuli Mia moja katika muda wa dakika ishirini.

Hatua hii imefanyika huku kukiwa na ongezeko la idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu Tanzania.

Tanzania ni miongoni nchi barani Afrika zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa huo na kutumia njia  hii katika kupambana na ugonjwa huu itakuwa ni afueni.
Wataalamu wanasema kuwa njia ya  hapo awali  ilitoa uhakika wa sampuli kwa asilimia 20 hadi 60 huko asilimia 40 hawagunduliki na hivyo kuendelea kuambukiza wengine.

Daktari Georgies Mgode  anasema mradi huo wa kupima vimelea vya kifua kikuu utakutumia panya waliofunzwa.
Dk.Mgode, ambaye pia ni meneja wa mradi huu, anafafanua kuwa panya hao wana uwezo wa kubaini harufu ya vimelea vya ugonjwa huo ndani ya sekunde.

Aidha, alisema  mbinu hii itakuwa mwafaka kwa wagonjwa na watafiti pia. Ishitoshe, muda utapunguka. Hapo awali kupima sampuli 100 kwa maabara zinazotumia hadubini kulichukua muda wa sikuu nne.Lakini sasa  mgonjwa atapata majibu ndani ya siku moja na kuanza tiba.

“Ni kweli hawa panya wana faida kubwa kwenye ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa wa TB, kwa sababu wana uwezo ndani ya sekunde wakabaini maambukizi ya kwa mgonjwa wakati mtu wa maabara anatumia zaidi ya siku moja kupata majibu,” alieleza Dk Mgode.

Alisema  maabara nyingine ya panya  buku iko mjini Morogoro ambayo hutumika kupima sampuli mbalimbali kutoka hospitali 28 nchini. Tangu mradi huo uanze kazi mwaka 2008 zaidi ya sampuli 380,000 zimeshapimwa.

Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP), Dk Allan Tarimo alisema Tanzania ni moja ya nchi zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa wa kifua kikuu barani Afrika ikiorodheshwa  ya nne huku kimataifa ikiwa nafasi ya sita.

Hakika hii ni hatua  kubwa ya kuokoa maisha ya wagonjwa na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo ambao ni changamoto Tanzania.

Kinaya  ni kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO)) linasema, kwa siku moja mtaalamu wa maabara anatakiwa kupima wagonjwa 20 tu wa kifua kikuu.


Jumatano, 23 Novemba 2016

Vasectomy

Uzazi mpango



Huku maisha yakiwa magumu Barani Afrika hususan Kenya, kuna haja yakufanya uzazi mpango ili kuweza kukimu mahitaji ya kila siku.

Akina mama kwa muda mrefu ndiyo wenye majukumu ya kupanga uzazi Huku Akina baba wakijihuzisha n'a majukumu mengine.

Lakini mambo imechukua mwelekeo mpya Huku wanaume wakiamua kupanga uzazi pia. 

Haya majukumu ni ya kila mmoja, n'a ni vema kushirikiana wake kwa waume.
Hii imepelekea wanaume kutafuta njia za kupanga uzazi.

Njia mojawapo ya hizo ni ile ya vasectomy; kufunga mirija unaotoa mbegu za kiume.
Hii ni njia ya kudumu ya kupanga uzazi.

Ni majuzi tu ambapo siku ya kuadhimisha uzazi mango wa vasectomy nchini Kenya n'a pia kote duniani. 

Nchini ya Kenya ilichukua fursa Hii kuelimisha jamii umuhimu wa wanaume kupanga uzazi.
Kadili ya wanaume hamsini walijitokeza kufajiwa upasuaji kubana mirija yao.
Hupasuaji huchukua muda wa nusu saa.

Hata hivyo kuna baadhi ya wanaume wanaokosoa shughuli Hii wakisema Hii ni tabia ambapo haiabatani na destuli za kiafrika. 
Wanasema haya ni mambo ya kizungu ambayo yanafaa kupakia na wazungu tu.
Wengine nao wanatoa maoni tofauti.

Wanaonelea ni vema kupanga uzazi wa vasectomy kwani unasaidia kupunguza majukumu, huku watoto wachache wakipata mahitaji yao bila shinda yeyote.
Wanasema ni vema wanaume kuwasaidia wake wao kupanga familia. 

Uchumi umezorota, watoto na jamaa kwa jumla wana mahitaji mengi .Wasipopanga uzazi basi wazazi watakuwa wanawaacha watoto wao kuumia.
Jambo muhimu la kufahamu ni kuwa njia hii;

*Haipunguzi hamu ya kufanya ngono
*Haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa.Hivyo basis ni vema kuchukua tahathali.
*Hali hii ni ya kudumu.Haitawezekana tena kupata watoto baada ya operesheni. 

Jumatano, 16 Novemba 2016

Conjoined twins -Kenya


Wataalamu katika hospitali kuu ya Kenyatta wamefanikiwa kuwatenganisha watoto mapacha walioshikamana kwenye sehemu ya mgongo.


Hiyo jana hospitali Hiyo ilitoa picha za watoto hao wakionana ana kwa ana kwa mara ya Kwanza. 



Ufanishi huu umetokea baada ya miaka miwili tangu kuzaliwa kwao.
Hii ni mara ya Kwanza madaktari katika hospitali Hii kuibuka na  ushindi kama huu.

Pia huu ni upasuaji wa kipekee kuwahi fanyika nchini Kenya.

Ilichukua muda na mpangilio wa hali ya juu kukusanya kundi la madaktari wenye ustadi katika maswala tofauti ya kiafya.
Watoto hawa walizaliwa na tatizo la kiafya ambalo kulitatua kwa haraka lingehatarisha maisha yao.

Hâta hivyo, kulikuwa na matumaini kuwa mafanikio ya kuwatenganisha yangepatikana.
Watoto Blessing na Favor walizaliwa miaka miwili iliyopita katika hospitali ya Mtakatifu Theresa,  Kiirua katika Jimbo la Meru.

Baadaya ya madaktari kushindwa kutatua hali yao kutokana na ukosefu wa vifaa au mashine za kisasa, walitoa rufaa hadi Hospitali kuu ya Kenyatta, Nairobi.
Daktari aliyeongoza upashuaji huu ni mashuhuri nchini Kenya kwa matibabu ya watoto.
Daktari Fred Kabuni, alisema ilichukua Masaaki ishirini n'a moja kufanya upashuaji huu.
Madaktari wengine walohusika ni mashuhuri katika taaluma tofauti ya kiafya. 
Wakenya walipongeza juhudi za wataalamu wa maswala tofauti ya kiafya waliojitolea kutekeleza shughuli hii ya kipekee.

Kathoni Kiama alisema"hii ni habari njema kwa Wakenya wote, kuona Kuwait madakari wetu wanawatenganisha watoto hawa.

Weru Kihiko anasema madakari wetu hongera kwenu."tunao madakari stadi lakini vifaa vya matibabu ni adimu.

Wafula David anasema madakari wetu wanajitolea lakini wanagoma kil a mara kutikana na mishahara duni. Ni heri selikali ingechukua hatua ya kuwalipa kulingana na kujitolea kuokoa maisha. 


Ufanishi huu unatokea huku wizara ya afya ikidaiwa kuvuja mamilioni ya pesa kwenye kafsha ya ufisadi.

Alhamisi, 29 Septemba 2016

Saratani ya tumbo


Aliyekuwa mtangazaji mashuhuli wa kituo change habari cha Royal Media Waweru Mburu ameaga dunia.

Waweru amefariki baadaya ya kuugua saratani ya tumbo.

Alitumika kwenye Radio Citizen kwa miaka zaidi ya kumi na tano, huku akiwa na umaarufu kufuatia kipindi chake cha yaliyotendeka.

Kabla yakufa kwake hiyo jana jioni, Waweru alitangaza nia yake ya kuwania kiti cha kisiasa katika eneo la maragua, jimbo la Murang'a.


 saratani ya  tumbo ni saratani inayotokea katika mfuko was chakula unaosiaga  na kutunza chakula kwa muda. Saratani hii hutokea  katika tezi za gastric gland.
Kulingana  na takwimu za afya,saratani hii inatokea sana katika nchi za Japani na China

Kinachosababisha saratani ya tumbo?

Wataalamu wa afya hawana uhakika nini husababisha saratani hii.Hata hivyo, Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya chakula kuchomwa, chenye chumvi nyingi au kilichohifadhiwa kwenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo..

 saratani ya tumbo  imepungua sana hasa sehemu ambapo matumizi ya friji inatumika kama njia ya kuhifadhi chakula.
 Duniani na kwa kiasi kikubwa

Kinacho changia saratani ya tumbo-gastric cancer?

Chakula chenye chumvi nyingi
Maambukizi ya bakiteria aitwaye helicobacter pyroli
Michomo ya muda mrefu tumboni(inflammations
Uvutaji wa sigara
Uvimbe kwenye kuta za tumbo kitaalamu stomach polyps

Dalili -tumbo-Gastric cancer

Kuhisi chakula kimejaa tumboni
Kichefuchefu na kutapika
Kushindwa kula chakula
Kushiba baada ya kula kidogo
Kukosa hamu ya kula
Kinyesi  cheusi au kuwa mweupe mikononi na chini ya kope kwa sababu ya upungufu wa damu
Kutapika damu
Kupungua uzito
Kuvimba tumbo aukupata uvimbe tumboni
Kuvimba mitoki san asana mitoki ya bega la kushoto na kwapani

Dalili za hatari

Kujaa maji kwenye mfuko unaofunika matumbo.
Kuziba kwa mshipa unaopitisha chakula kutoka kwenye tumbo na  husababisha chakula kujaa tumboni
Kukonda sana kutokana na saratani au kukosa hamu ya kula

Ijumaa, 5 Agosti 2016

breastfeeding week



Image result for breastfeeding month 2016 WHOmaziwa ya mama ndicho chanzo bora zaidi cha lishe kwa watoto wachanga,hata hivyo kuna badhi ya akina mama ambao hawapendi kamwe kuwanyonyesha watoto wao kwa sababu za kutaka kuhifadhi umbo la titi.


Lakini mashirika ya kiafya yanaendelea kuwahimiza akina mama kuwanyonyesha watoto ili kuepuka maradhi na kumpa moto afya bora .

Image result for breastfeeding World heath org
Pia ni muhimu kwa  akina mama ili kuepuka maradhi kama vile saratani ya titi au maradhi mengine  kama vile msongo wa mawazo ambao hupata akina mama wengi baada ya kujifungia.


Kulinga na utafiti wa WHO ambayo imetolewa kwa ajili ya wiki ya kunyonyesha duniani ,  ni nchi chache tu ambazo hutekeleza mfumo wa kimataifa, unaolenga kuzuia matangazo ya lishe mbadala kwa watoto.


Akina mama ambao hufanya kazi hasa katika mashirika tofauti huwa na ungumu wa kupata muda wa kunyonyesha ,jambo ambalo huwachochea akina mama kununua na kuwapa watoto wao vyakula vya mikebe. 


Isitoshe,maziwa ya mama ni muhimu zaidi kumjenga motto kimwili na pia kiakili.Hivyo basi ni vema kumnyonyesha mtoto kuliko kutengemea maziwa ya mbadala.

Image result for breastfeeding drawingEndapo watoto wa miezi 0-23 wangepata maziwa ya mama basi 800,000 wangeokolewa kila mwaka.


Jinsi ya kunyonyesha


  • Anza kunyonyesha baada ya saa moja ya kuzaa (unyonyeshaji wa mapema)
  • Usimptie mtoto chochote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza (unyonyeshaji wa kipekee)
  • Usimwage maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaa, huwa na protini na kingamwili ambayo ni muhimu kwa mtoto mchanga. Unapaswa kumwambia mama amlishe nayo mtoto mchanga, kwa sababu ni ‘chanjo’ ya kwanza ambayo mtoto atapata.
  • Keti kwa hali nzuri wakati unanyonyesha
  • Hakikisha mtoto anapata vizuri matiti ya mama anaponyonya
  • Hakikisha mtoto ananyonya vizuri

KAMPENI YA WHO itaendelea hadi tarehe saba Augusti kwa malengo ya kuwaelimisha akina mama umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.




Alhamisi, 21 Julai 2016

Tohara Kenya



Huku baadhi ya kabila nchini Kenya zikiendelea kupasha tohara wasichana,shirika la umoja wa mataifa limetaja kitendo hikikama dhuruma kwa watoto.

Daktari Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa UNPF ametaja ukeketaji kama kitendo cha unyama na dhuruma kwa mtoto.

Alisema kuna haja ya wadau kutafuta mikakati itakayo hakikisha unyama huu imekomeshwa katika sehemu au mataifa yanaoendelea kutekeleza uovu huu,hasabara la afrika abako takwimu zinaonyesha hali ni mbaya.

Mataifa ya jamhuri za kiislamu,Afrika Mashariki,Magharibi na Kusini ni baadhi ya maeneo ambayo yangali yanakubatia mila na tamaduni potovu za ukeketaji.

Alisema shirika lake linatafuta mikakati na sheria ya kuhakikisha swala hili limekomeshwa kabisa.

Hii ni baada ya muda wa miaka ishirini ambapo mashirika ya kiserikali nay ale ya haki za kibinadamu yakikasifu tabia ya ukeketaji barani Afrika .

TB kenya



Kiwango kikubwa cha  watu wanaogua ugonjwa wa kifua kikuu wamekuwa  wakipatikana  na Virusi Vya Ukimwi.Aidha kuchangia vifo miongoni mwa waadhiriwa.

Juhudi za kupambana na TB na maambukizi ya Ukimwi zinaendelea  barani Afrika hususan nchini Kenya.

Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kifua kikuu kama moja wapo wa magonjwa ambukizi yanayosababisha maafa nchini. Kesi za kifua kikuu zimeongezeka Zaidi ya mara tatu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Mwaka wa 2015 Zaidi ya watu elfu kumi walifariki kutokana na makali ya TB.

Jimbo la Pwani ya Kenya linaongoza kwa idadi ya maambukizi ya kufua kikuu huku Nairobi,Isiolo,Kisumu na Embu zikifuata.
Vile vile,Majimbo ya Samburu,Tharaka,Turkana na Kirinyaga zina idadi ya azili mia 32 ya maambukizi.

Kenya imekuwa mtari wa mbele kuuthibiti ugonjwa wa Tb lakini changamoto zikiwemo wagonjwa kukataa ktafuta matibabu au kukata kumeza dawa.
ilibidi serikali kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha kwa hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wanaokataa kumeza dawa.
Hata hivyo kutiwa nguvuni waliokiuka maagizo ya daktari yalikosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Hiyo pia ni changamoto kwani sheria au sera za afya na wagonjwa pia sharti kiundwe na kulindwa.

Uganda,Tanzania na Zimbabwe bado zimeonekana kushindwa kukambiliana na tishio la TB

Hivi majuzi,serikali ya Kenya  ilizidua  mradi: mulika TB,Maliza TB kama moja wapo wa juhudi za kutokomesha ugonjwa huu nchini.

Jumatatu, 18 Julai 2016

AIDS CONFERENCE DURBAN 2016

Kongamano la tano la kimataifa kuhusu ukimwi kuanza Afrika Kusini

Kongamano kuhusu ukimwi liaanza  mjini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wajumbe na wataalam kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Mkutano huo unafanyika wakati ambapo  selikali ya Kenya imejitahidi kukabiliana na makali yake.


 Siku chake zilizopita, wizara ya afya Kenya, ilianzisha sera na kampeini ambayo itawasaidia wanaougua na  wanaofahamu hali yao ya HIV kupata tiba mara moja.Kampeini inayo ;anza sasa pia itawezesha watoto wanaozaliwa na virusi vya HIV kuanza matibabu mara moja.
Kenya unveils national initiative to scale up HIV testing and treatment
 Lakutia moyo ni kwamba  idadi ya maabukizi nchini Kenya imepungua,huku Afrika kusini hasa Durban ambapo mkutano huu unafanyika hali ikiwa sio nzuri.

 Zaidi ya hayo,Utafiti unaonyesha  watu milioni 40 ulimwenguni walioambukizwa virusi vya ukimwi wanatokea barani Afrika.

 Serikali ya kenya imetenga shilingi bilioni 22 kupambana na janga hili la Ukimwi huku shilingi 15,000 zikitengwa kwa kila mgonjwa ili kumwezesha kupata dawa za ARV.

 Hii ni binu mwafaka kwani hali  ya kimaisha kwa waadhirirwa itaimarika maradhufu.

Lengo kuu la mkutano wa Durban ni kutathmni tafiti za  kisayansi kuhusu matibabu, dawa na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya ukimwi.
 Mbali na huduma nzuri zinazotolewa na mataita mengi ili kudhibiti ukimwi,Changamoto ya bado zipo. Unyanyapaa miongoni mwa wagonjwa wengi wa ukimwi, Majibu yanapobainisha wana virusi vya ukimwi; hawajui wafanye nini au waanza vipi kutumbia tembe.

Hivyo basi,itakuwa ni jambo la kutia moyo baada ya mkutano wa Capetown kukamilika.
  Wataalam na watafiti wa maswala ya afya , mchango wao utazaa matunda  katika kuboresha huduma za matibabu na kupata mbinu  ya watu wanaoishi na virusi vya HIV na wagonjwa wa ukimwi bila kutengwa.
Kongamano hilo ambali, hufanyika kila baada ya miaka miwili na huwavutia wajumbe takriban 5,000 kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni kote. Wanasayansi, madaktari, watalaam wa afya ya umma na viongozi wa kijamii ni pamoja na wanaohudhuria kongamano hili.

Kongamano la awali lililofanyika Australialilikubwa na husuni na kilio baada ya watafiti wa ukimwi kufariki katika ajali ya ndege.


Jumanne, 10 Mei 2016

homa ya mapafu(Pneumonia)

Pneumonia


Homa ya mapavu ni ugonjwa ambao unaathiri mapafu na unaua watoto kwa wingi hasa katika nchi zinazoendelea duniani.

Ugonjwa wa nimonia umetajwa kuwa ugonjwa hatari na unauwa kwa kasi sana,huku idadi ya maafa yakiongezeka kila siku. nchini Kenya.

Ripoti ya wizara ya afya ,Kenya inasema kuwa idadi ya wanaofariki imeongezeka maradufu.


Pia watoto wameathirika Zaidi,inakadiriwa kwamba watu karibu 21,640 walifariki mwaka wa  2013 huku idadi ikiongezeka hadi  22,473 mwaka uliopita wa 2015.

Hii ni changamoto kwa sekta ya afya kwani kuna mbinu za kupunguza makali ya nimonia.
 vifo hivi vinavyotokana na homa ya mapafu(nimonia) ,vinaripotiwa wakati madaktari na wauguzi wamekuwa wakifanya migomo kulalamikia mishahara duni na pia mazingira mabaya ya kufanyia kazi.
Image result for pneumonia
Hii ni jambo ambalo si la kuchangamkiwa ,na ni sharti wizara ya afya itekeleze majikumu yake ipasavyo.

Ni husuni kusuhudia maafa ya kila mara ,hasa kwa wazazi katika sehemu za majimbo ambako hali ni mbaya Zaidi.
mwezi uliopita,jimbo la Nakuru lilikuwa na idadi kuwa ya maabukuzi na maafa ya ugonjwa huu.


kwenye kaunti ya Nakuru , watoto takriban 20 waliaga dunia kutokana na ugonjwa wa Pneumonia katika kipindi cha mwezi mmoja.
Waziri wa afya kwenye kaunti hiyo Mungai Kabii alisema kesi zingine 117 ziripotiwa kwenye vituo vya afya kadhaa kwenye eneo hilo na pia kwenye kaunti zingine jirani.
Kufuatia mkurupuko huu, sampuli ya damu kutoka kwa walioathiriwa zimetumwa kwenye maabara za shirika la KEMRI ili zifanyiwe utafiti huku wauguzi wakitafuta  namna na mbinu za kuudhibiti,
Alisema watoto wenye umri wa kati ya siku moja na miezi kumi na moja ndio wako katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa.
Dalili za nimonia 
 Joto kupanda, kutokwa na jasho unyonge wa mwili pamoja na kukohoa,homa,kuhisi baridi,kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua,kushindwa kunyonya na kula,mtoto kubadilika rangi ya bluu midomo,kuumwa na tumbo na kutocheza.
Homa ya mapafu husababishwa na nini?

Aina ya vimelea kama vile bakteria,virusi,parasite na fangasi.
Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na pia mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi.
 
Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara .
 

 

 

 

Jumatano, 27 Aprili 2016

Malaria Kenya


Idadi ya wagonjwa wa  malaria yapungua Kenya

Ugonjwa wa malaria umekuwa ni tisho katika maeneo yenye joto Afrika hususan nchini Kenya.
Image result for malaria mosquito kenyaJambo la kutia moyo ni kwamba  iadadi ya watu wanaougua ugonjwa huu umepungua marudufu kwa miaka sita iliyopita.

Kulingana na tafiti za wizara ya Afya hali hii inatokana na ongezeko la utumiaji viandarua na pia kupata matibabu mapema.Msemaji wa wizara ya afya Elisha Omondi anasema hatua za serikali za kuukabili ugonjwa wa malaria zimezaa matunda.
Hata hivyo sehemu kama vile  jimbo la Siaya linaongoza kwa maambukizi hayo,lakini pia katika kipindi cha mwaka mmoja angalau asilimia 50 ya visa vimekabiliwa.
Majimbo ya Pwani pia yameadhirika lakini hali sio mbaya kama siku za nyuma.
Takwimu sinaonyesha kuwa Malaria iliwaua karibu watu nusu milioni duniani mwaka jana, huku vifo tisa juu ya kumi vikitoka kusini mwa Sahara.
Kenya ni miongoni mwa mataifa ya kusini mwa Jangwa la Afrika ambapo Malaria imeandelea kuangamiza watu lakini hali hii imeimarika  kwa asili mia nane ikilinganishwa na hali ilivyokua miaka sita iliyopita.
Isistoshe, wanawake waja wazito na watoto wako hatarini zaidi na wanatakikana  wanapokea matibabu punde zinapojitokeza dalili za ugonjwa kwani.

Mama Lucy KIbaki

Aliyekuwa mama wa taifa Aaga dunia


Baada ya kifo chake aliyekuwa Mama wa taifa nchini Kenya,watu wa tabaka mbali mbali wameendelea kutakia familia yake afueni,huku wakimumiminia sifa kama mama wenye bidiina aliyewajali wasiojiweza.

Juhudi zake za kuunda muungano wa akina mama wa marais afrika ili kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ni mfano wa mama aliyewajali wengine.

Pia alikuwa mstari wa mbele kuhakikisa maswala na afya ya uzazi imeimarishwa.Aliwatembelea wagonjwa hospitalini na aliyoyaona hasa mazingira mbaya wagonjwa waliokuwemo yalimtamausha.


Alinena kwa hasira na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa maafisa wa selikali wafisadi .

Hospitali ya mama Lucy ilijengwa kwa heshima zake na wakaazi wa Embakazi wana sababu kushukuru kwa hayo."ukakamavu wake mama na bidii katika maswala la afya ilifanya sisi tupate hospitali karibu,tunafurahi sana,alisema Monica Wahito .

John Kariuki anasema ,''hospitali ya mama Lucy imekuwa na sifa mbaya ya kutekelezwa kwa waogojwa na jambo hili ni sharti libadilike kwa heshima ya mama Lucy Kibaki.
Alifanya mambo mengi ambayo tutamkumbuka.

Haijabainika alikokuwa akiugua .Kwa muda mrefu wakenya wamekuwa wakitaka kujua hatima yake ,kwani ajaoneka kwa miaka karibu sita.

Mama Lucy amekuwa akiuguakwa muda .Alilazwa katika hospitali moja hapa nchini Kenya hadi alipohamishwa jijini London kwa matibabu ya dharura hadi kufariki kwake hapo jana.

Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.

Jumanne, 8 Machi 2016

Josephine Nyambura aaga duniani cancer


Maoni
Ugonjwa wa saratani waendelea kukusababisha maafa.

Idadi ya wanaofariki kufuatia maradhi hayo yanaongezaka kila kuchao. 
Ni hali ya kuhuzunisha kuona kuwa Wasio na uwezo wa kugharamia matibabu ndio wanaoadhirika zaidi. 

Ni jukumu la serikali kutafuta mikakati ku
ona kwamba watu wote wanapata matibabu bila vikwazo vyovyote.
Huduma ya bima ya kitaifa inapashwa pia kusaidia wenye uwezo wa kulipa malipo ya kila mwezi na pia wasioweza. 



Malkia Josephine Nyambura aaga duniani.

Mtoto wa miaka nne ambaye hivi majuzi alikosa kupata matibabu ya ugonjwa wa saratani kufuatia matatizo ya kifedha yaliyoikuba familia yake aaga duniani. 

Malkia Josephine Nyambura alinyimwa matibabu na madaktari nchini India na kwa kuwa hali yake ilikuwa hatarini wawazi   wake wakamrejesha nchini Kenya katika hospitali kuu ya Kenyatta ambayo pia Imekuwa na upungufu wa mashine za saratani. 
Hali yake ilizorota baadaye huku mwili wake kufula.

Saratani ya damu aliyokuwa akiugua mtoto inaweza tibia kwa asilimia 70 hasa nchini India , kutoka na vifaa vya kiteknologia vinavyotimiwa,  ikilinganishwa na hapa nchini Kenya. 
Gharama ya matibabu ya saratani ni ghali mno na kwa familia hii kwa upendo wa mwanao waliuza mali yao yote ili mtoto wao apate matibabu , lakini hata baada ya hayo yote.

Gharama iliendelea kuwa kikwazo hadi wakalazimika kukatiza matibabu huko India. 
Kabla ya kufarikiyule,Malkia b alimhakikishia babake kuwa hatafarki kama njia moja ya kuwaongezea matumaini wakazi wake walioonekana kuhuzuniswa na hali yake. 

Jambo la kutamausha ni kuwa hata baada ya habari za mtoto Malkia Nyambura kuangaziwa na vyombo vya habari hatua za kutafuta pesa za matibabu hazikufua dafu.
Imekuwa ni safarini yenye Milima na mabonde kwa mtoto na wazaziwe .

Mola awape amani familia yake Malkia na wengine wanapitia hali hii ngumu.

Malkia lala salama. 

Ijumaa, 4 Machi 2016

ZIka Chanjo -Vaccine


Huku ugonjwa wa Zika ukiendelea  kuenea kwa kasi,kampuni ya  dawa ya ufaransa -Sanofi Pasteur iko katika harakati  na shughuli za kukomesha virusi vya Zika.
Kwa sasa kuna mikakati ya kufanya utafiti wa chanjo kwa binadamu ili kuepuka adhari za ugonjwa wa Zika.
Image result for zika vaccineKulingana na Nicholas Jackson, ambaye anaongoza kundi la watafiti ,shabaha yao ni kuhakikisha wamepata tiba ya virusi vya Zika haraka iwezekanavyo.
Ingawa utafiti wa chanjo huchukua muda- mrefu,miaka ishirini na zaidi- kundi hili lina matumaini  kuwa watafanya wawezalo kuhakikisha tiba imepatikana kwa muda mfupi.

Zaidi ya hayo,Mtafiti Jackson,ananukuliwa akisema ,kampuni ya Sanofi Pasteur inaweza kutumia ufundi,vifaa na uzoefu vilivyotumia katika utafiti na utengenezaji wa chanjo ya virusi ya Dengue miaka kadha iliyopita,katika shughuli  za utafiti na chanjo ya virusi vya Zika.

Kampuni hiyo ina umaarufu na pia  inaongoza duniani katika utafiti wa chanjoya virusi vya Homa ya Majano.Chanjo yake ilipata kibali cha kutumiwa katika nchi za Brazil,Mexico na ufilipino.
Sanofi  imechukua hatua ambayo  tayari kampuni zingine za dawa kama vile;  Bharat Biotech ya India,  Inovio naTaasisi ya afya ya kitaifa ya Marekani(  U.S. National Institutes of Health) -kampuni za marekani  zimezindua utafiti wa tiba ya Zika.
 Jaribioya chanjo hiyo kwa binadamu henda ikawa mwaka ujao,ikiwa mikakati iliowekwa itafikiwa bila shida yeyote.
Haijabainika hakika ikiwa virusi vya Zika vinasababisha motto kzaliwa na kichwa kidogo ,lakini kuna uhusiana wa kuabatanisha hali hiyo na virusi hivyo.
Shirika la Afya Duniani(WHO) linakisia kuna idadi ya 15 kampuni na wasomi ambao kwa sasa wanatafiti tiba ya Zika.

Jumatatu, 15 Februari 2016


Masaibu ya wagonjwa katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki

Mama Lucy Kibaki hospitali iliyoko Embakasi imegonga vyombo vya habari kwa sababu za kuhuzunisha.

Image result for mama lucy hospitalHuduma duni za matibabu,ufisadi ni baadhi ya madai yanayotolewa na wagonjwa ambao wameadhirikakwa njia moja au nyingine.

Visa vya wagonjwa kutohudumiwa ipasavyo na madai ya ukosefu wa vifaa vya matibabu vinahusunisha.

Kisa cha kustajabisha ni kuwa madaktari walimwacha mama mja mzito bila kuhudumiwa kwa muda hadi wanawe mapacha kufia kwenye kizazi.

Imedaiwa kuwa mtoto aliyekuwa na majeraha ya ajari aliruhusiwa kwenda nyumbani hata kabla ya uchunguzi wa kina kuhakikisha kuwa maisha yake hayakuwa hatarini

Mamake mtoto anasema mwanawe aliaga dunia siku oja baada ya kwenda nyumbani.

Baadaye daktari katika hospitali hiyo wakamfahamisha kuwa alivuja damu kwa ubongo,kwani alikuwa na majeraha jichoni.

Hayo ni baadhi ya masaibu yanayowakuba wagonjwa kwenye Hospitali ambayo ni ya pili kwa ukubwa jijini Nairobi na ya tatu nchini.

Madhumuni ya kuanzisha hospitali hii ilikuwa kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa katika hospitali kuu ya Kenyatta